Friday, February 25, 2022

WAWEKEZAJI WA DUBAI WAHAKIKISHIWA USALAMA NA ZIC

    Na. Khadija Seif, Michuzi TV

MAONESHO ya Biashara Kimataifa ya Expo Dubai yanayoendelea katika Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) linawakaribisha  Kuwekeza Visiwani Zanzibar kwa Uwekezaji  na Kuwahakikishia usalama wa uwekezaji na Mali zao wakati wote wakiwepo Visiwani humo. 

Akizungumza katika maonesho hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la (ZIC) Arafat Haji amewakaribisha wadau Kuwekeza Visiwani Zanzibar na kupitia Shirika hilo linawahakikishia usalama wa uwekezaji wao kutokana na Shirika hilo kuwa na uzoefu na masuala ya bima za aina mbalimbali.

"Wawekezaji tunawapa Elimu ya namna gani wataweza kuwa na uwekezaji wenye usalama na kuhakikisha kunakua na Ajira ya Muda mrefu Ili kuleta tija na kukuza uchumi na maslahi ya Taifa."

Aidha, Haji ameeleza kuwa wawekezaji wanapoamua kushirikisha (ZIC) wanafanya maamuzi sahihi kwani wapotayari kuwapa Miongozo ya kusimamia uwekezaji huo na kuhakikisha Mitaji yao inaleta Manufaa.

No comments :

Post a Comment