Saturday, February 19, 2022

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUZINDUA CHUO CHA SIASA CHA MWALIMU NYERERE KIBAHA

 Na Khadija Kalili, Pwani

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua Chuo Cha Siasa Cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha Kwa Mfipa Mkoani Pwani uzinduzi umepangwa kufanyika Februari 23 jumatano  mwaka huu.



Akizungumza leo  katika  mkutano na  Waandishi wa habari  wa  Mkoa wa Pwani  Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge alisema kuwa  hali ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa iko vizuri huku akitanabaisha kuwa  wakaazi wa Mkoa huu  wajitokeze kwa wingi Ili kutoa hamasa ya uzinduzi huo.

"Nimewaita ili   niueleze  umma  kwa kupitia ninyi kuwa Mheshimiwa Rais wetu wa awamu ya sita Mama Samia Suluhu Hassan atafanya zaiara Maalumu  katika Mkoa wa Pwani  ambapo atakuja mahsusi kwa kufanya uzinduzi  wa Chuo hiko ambacho kinamilikiwa na  Chama Cha Mapinduzi (CCM)  pia ikiwa na vyama vyote  vingine vya siasa  barani Afrika ambavyo vilikuwa katika mstari wa
mbele wa ukombozi wa nchi zao alisema RC Kunenge.

RC. Kunenge aliongeza kwa kusema kuwa    "wakaazi wa Mkoa wa Pwani tumepata heshima  hivyo tujitokeze   kwa wingi kuja kumlaki Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan " alisema .

Awali RC Kunenge alisema kuwa  Februari 22 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo kwa kushirikiana na Makatibu  Wakuu wanne  wenzake kutoka katika vyama vingine ambavyo  vilipigania uhuru wa nchi zao   huku majina na nchi zake kwenye mabano ni ANC (Afrika ya Kusini) FRELIMO (Msumbiji) , SWAPO (Namibia) na ZANU PF ( Zimbabwe) , NPLA  (Angola)  wote kwa pamoja  watazindua barabara  yenye urefu wa Kilometa mbili inayokwenda chuoni hapo.

No comments :

Post a Comment