Saturday, February 19, 2022

NIMR WAMLILIA DKT. MWELE MALECELA


TAASISI ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) wamlilia Dkt. Mwele Ntuli Malecela leo Febuari 19, 2021 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kuaga mwili wa marehemu Dkt. Mwele, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu), Profesa Yunus Mgaya amesema kuwa Dkt. Mwele, NIMR alifanya kazi kwa Miaka 30, atakumbukwa kwa mpango wa

kudhibiti magonjwa mawili.

Amesema kuwa Mwele atakumbukwa kwa kuanzisha mpango wa Kidhibiti magonjwa yasiyoambukiza ya Matende na mabusha na aliendesha programu hiyo kwa ufanisi Mkubwa na umahili wa hali juu.

"Ndiye aliyesababisha Wizara ya afya ihuishe mpango wa kudhibiti magonjwa yalikuwa hayapewi kipaumbele".

Prof. Mgaya amesema kuwa mpango huo baada ya kukamilika ulijumlisha magonjwa matano yaliyokuwa hayapewi kipaumbele nchini na kuanza kuyafanyia utafiti wa kuyatibu.

Amesema kuwa kazi ya Dkt. Mwele alihakikisha kwamba magonjwa matano yasiyopewa kipaumbele yanatokomezwa hapa nchini.

" NIMR tutaendeleza ndoto ya Dkt. Mwele kuhakikisha haya magonjwa matano yasiyopewa kipaumbele yanadhibitiwa nchini." Amesisitiza Prof. Mgaya

"Tunaungana na waombolezaji wote kumpa pole nyingi Mzee John Malecela na familia yote kwa ujumla kwa msiba huu kwa kuondokewa na mpendwa wetu sote." Ametoa pole Prof. Mgaya

Dkt. Mwele (58) alifariki dunia Februari 10 mjini Geneva, Uswisi wakati akiendelea na matibabu, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, na alikuwa Mkurugenzi wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

 









No comments :

Post a Comment