Mahakama ya Tanzania na Ubalozi wa Uingereza kuendelea kushirikiana kuwajengea uwezo zaidi Mahakimu na Majaji ili kuboresha utoaji haki katika taasisi hiyo.
Hayo yamesemwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof Ibrahim Juma wakati akifungua mkutano wa kubadilishana ujuzi baina ya majaji wa nchi hizo mbili uliofanyika Januari 31, jijini Dodoma.
Jaji Mkuu amesema, serikali ya Uingereza imekuwa ni mdau mkubwa katika maboresho ya utoaji haki nchini ambapo serikali hiyo imeiwezesha mahaka kutengeneza muongozo wa kutoa adhabu.
“Swala la adhabu ni swala ambalo linazungumzwa sana. Na Serikali ya Uingereza kupitia Ubalozi wake hapa nchini ulitusaidia kuweza kutengeneza muongozo wa kutoa adhabu.
Muongozo huo unawasaidia Mahakimu na Majaji wasitoe adhabu zinazotofautiana sana katika kosa linalofanana. Na huo ni mfano wa ushirikiano baina ya Mahakama na Serikali ya Uingereza kupitia Ubalozi wake hapa nchini.” amesema Prof Ibrahim.
Kwa upande wake Balozi wa Uingereza nchini, David Concar amesema serikali yake itaendelea kusaidia katika maboresho ya mahakama zote mbili, ya Zanzibar na Tanzania Bara ili kuchagiza utoaji haki wa haraka na haki.
No comments :
Post a Comment