Wednesday, January 5, 2022

Bodi Ya REA Yajiridhisha Na Mradi Unaozalisha Umeme Mwingi Kuliko Mahitaji Wilayani Ludewa

Baadhi ya wajumbe wa bodi ya REA wakikagua sehemu ya mto ambako mitambo ya mashine za kufua umeme wa maji wa kampuni ya Madope imefungwa wilayani Ludewa.

B:Wajumbe wa bodi wakipata maelekezo ndani ya Power house katika kampuni ya kufua umeme ya Madope Hydro Company Limited.
Na Amiri Kilagalila,Njombe


Serikali kupitia wakala wa nishati vijijini (REA) umetoa ruzuku ya fedha Milioni 300.5 kwa kampuni ya uzalishaji umeme ya Madope Hydro Company Limited iliyopo Ludewa mkoani Njombe ili ziweze kusaidia katika uunganishaji kwenye line ya TANESCO kupunguza changamoto ya ukatikaji wa umeme kutokana na uzalishaji mkubwa wa nishati katika kampuni hiyo.

Akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua mradi huo uliopo kata ya Lugarawa wilayani humo mhandisi Styden Rwebangira kwa niaba ya wajumbe wa bodi amesema,wateja wamekuwa wakikosa umeme wa uhakika kutokana na changamoto ya kukatika mara kwa inayotokana na mitambo mikubwa inayozalisha imeme mwingi kuliko mahitaji.

“Ambacho tumegundua ni kwamba mtambo ni mkubwa,lakini matumizi ni madogo sana kiasi kwamba mtambo unatembea kwenye chini ya asilimia 50 ya uwezo wake kwa hiyo hali hiyo imekuwa inapelekea mtambo unakata mara kwa mara”alisema Rwebangira

Aidha amesema ili kutatua changamoto,serikali imetoa kiasi cha fedha ili pia kuunganisha kiasi hicho cha umeme kwenye line ya TANESCO kwasababu ina mahitaji makubwa.

“Hizo fedha tulishazitoa kwa hiyo kilichotuleta leo ni kuja kuangalia fedha zimetumika vipi,tumetoa milioni 300.5 kwa ajili ya kuunganisha na line ya TANESCO,na kwa ajiri ya kuunganisha vijiji 15 tumewapa URO milioni Mbili”aliongeza Styden Rwebangira

Kulwa Masanja ni mhandisi wa mradi huo,amesema umeme unaozalishwa ni Megawati 1.7 unaosambazwa kwa vijiji 20 kwa sasa na wamebakiwa na vijiji viwili vya Utilili na Lusala ambavyo bado kuvifikia kutokana na Changamoto zilizo nje ya uwezo wao.

“Tunashukuru REA wamekuja kwa ajili ya kusaidia kutatua baadhi ya Changamoto na changaomto kubwa tuliyo nayo ni miundombinu lakini pia kuna vitongoji vingi ambavyo bado hatujavifikia na sasa wamekuja kutuongezea Nguvu”alisema Kulwa Masanja

Baadhi ya wananchi wa Lugarawa wilayani humo akiwemo Solomon Mgimba na John Mlowe wanasema katika maeneo yao wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kukatika kwa umeme mara kwa hali inayowaafya kuwarudishia nyuma maenedeleo na wanaiomba serikali kuwasaidia ili kutatua changamoto hiyo.

No comments :

Post a Comment