Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF) Angelina Ngalula akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na TPSF ilivyojipanga kuelekea uwekaji wa bomba la mafuta kati ya Tanzania na Uganda.
*Yataka kuweka mnyororo kuunganisha wafanyabiashara wadogo na wa kati
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
TAASISI ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF) imesema kuwa ujenzi wa Bomba la Mafuta kati ya Tanzania na Uganda unaanza hivi karibuni kutokana na mkataba mwisho kusainia kwa kwa nchi mbili hizo hivyo wafanyabiashara wanatakiwa kuwa na kampuni imara zenye viwango vya kimataifa pamoja na kuwa mnyororo wa wafanyabiashara wadogo kwenye ushindani wa zabuni zitakazotolewa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 2,2021 Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Angelina Ngalula amesema kuwa katika biashara zipo fitina nyingi kazi ya kufanya ni kuimarisha kampuni ziwe zina uwezo kutokana na vigezo vilivyoanishwa.
Amesema kuwa kwa upande uchomeleaji wa mambomba ni wakati wenye kampuni kupekeka vijana wakapate mafunzo TRIDO ambapo watapata vyeti ndivyo vitambulika na wakati ukifika wa zabuni rahisi kupiganiwa.
Angalula amesema bila kuimarisha kampuni za ndani kazi hizo zitaonekana kwa wafanyabiashara wa nje na kubaki kuona magari yao yakipita na hakuna mtu wa kulaumiwa kutokana na wazawa kushindwa kujipanga kimkakati wa kuzipata fedha nyingi zilizo kwenye mradi huo.
Mwenyekiti Amesema kwa mradi wa wafanyabiashara tunatakiwa kubebana kwa kuwa na mnyororo wafanyabiashara wadogo na wa kati.
Aidha amesema kuwa kazi hizo ni zile kampuni zenye viwango vya kimataifa hivyo kwa Kampuni za ndani zijijenge kufika viwango ambapo kwa miradi ya serikali ni rahisi kuchikuliwa.
Ngalula amesema kuwa katika mradi huo maeneo 13 wamepangiwa hivyo ni fursa ambapo kunahitaji kujipanga kwani kutakuwa na ushindani kwa vigezo vilivyowekwa.
No comments :
Post a Comment