Thursday, December 2, 2021

SHUHUDA WA MATUMIZI YA ARV ASISITIZA MATUMIZI SAHIHI YA DAWA KWA WATUMIAJI

Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Ahmad Abbas akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani ambayo katika mkoa wa Pwani yamefanyika katika Wilaya ya Kibiti.
Program Meneja wa  wa Mkoa, Dkt.Rehema Msimbe  akizungumza kuhusu takwimu za mambukizi ya UKIMWI katika mkoa wa Pwani wakati wa maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani.
Shani Shaban Mbonde akitoa ushuhuda kuhusu matumizi ya dawa ya ARV

Na Khadija Kalili,Kibiti

Mkaazi mmoja  la Kibiti Mkoa wa Pwani aliyejitambulisha kwa jina la Shani Shaban Mbonde (60) ametoa shuhuda yake ya kutumia dawa hizo kwa muda wa miaka 25 huku akiwasisitiza vijana nawatu wengine  kupima ili kuweza kutambua afya zao na pindi watakapokuwa wameadhirika basi wazingatie matumizi ya dawa hizo.

Mbonde alisema hayo kwenye maadhimisho yaliyofanyika Kibiti Mkoani hapa ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu Wa Wilaya ya Kibiti Kanali Ahmad Abbas  ambaye alikuwa akimuwakilisha  Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge aliyekuwa na udhuru.

Dkt.Rehema  Msimbe ambaye  ni Meneja  Program  alisema kuwa kiwango cha maambukizi mapya imepungua katika Mkoa wa Pwani huku wanawake wakiongozwa kwa idadi ya kupima ikilinganishwa na wanaume.

Akizungumza kuhusu utoaji wa huduma kwa wateja wao amewataka  wataalamu  kuwa na Lugha za staha  kwa sababu UKIMWI bado ni janga la Dunia na Taifa kwa ujumla hivyo Kila mtu achukue tahadhari huku akisema kuwa   watu wakapime Ili waweze kujitambua  na Njia ya kuishi ipo.

Alisema kuwa mwaka huu kuli mbiu inasema zingatia  Usalama Tokomeza UKIMWI Tokomeza  magonjwa ya mlipuko.

No comments :

Post a Comment