Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Bw. Tixon Nzunda akitoa hotuba ya ufunguzi rasmi wa mafunzo ya tathmini za ulemavu na magonjwa yatokanayo na kazi kwa madaktari na watoa huduma za afya kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini jijini Mbeya Novemba 30, 2021. Mafunzo hayo yanaratibiwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF). Wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma (katikati) na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tthmini, Dkt. Abdulsalaam Omar.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, akitoa neno la utangulizi.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, akifafanua kuhusu mambo ya kuzingatia wakati wa kufanya tathmini.
NA K-VIS BLOG, KHALFAN SAID, MBEYA
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Bw. Tixon Nzunda, amewataka madaktari wanaopatiwa mafunzo ya jinsi ya kufanya tathmini za ulemavu na magonjwa yatokanayo na kazi (impairment assessment of occupational accident and diseases) kufanya kazi hiyo kwa weledi na kuzingatia maadili.
Bw. Nzunda ameyasema hayo jijini Mbeya, wakati akifungua mafunzo ya siku tano yanayoratibiwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ambapo madaktari na watoa huduma za afya wapatao 100 kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambayo ni Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Ruvuma, Njomba na Iringa wanashiriki.
“Watakati wote mnapswa kuzingatia misingi mitatu wakati mkitekeleza majukumu yenu, weledi, uadilifu na uwajibikaji,” alisema Bw. Nzunda.
Alisema kosa lolote dogo (any slight error) litakalofanywa katika kazi ya kufanya tathmini ya ulemavu na magonjwa yatokanayo na kazi litapelekea athari katika maisha ya watu, uchumi wa nchi na kuhujumu Mfuko.
Aidha alisema lengo la Serikali la kuanzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni kuhakikisha wafanyakazi wanapata Mafao bora tofauti na sheria ya zamani ya fidida kwa wafanyakazi ambapo huko nyuma fidia ya juu iliyokuwa ikitolewa kwa mfanyakazi aliyepata ajali kazini au magonjwa yatokanayo na kazi ilikuwa ni kati ya shilingi 108,000/= na 80,000/= mtawalia.
Akitoa neno la ukaribisho, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma alisema katika kuhakikisha Mfuko unafanya jukumu lake kubwa la kutoa fidia kwa wale ambao wanapatwa na majanga wakiwa kazini ni vema tathmini zikafanyika kwa usahihi na kwa haraka.
“Hili la usahihi lina maanisha tunahitaji kushirikiana na wenzetu hawa ambao tayari ni wataalamu katika maeneo hayo na hili la uharaka lina maanisha Mfuko hauwezi kuwa na madaktari kila kona ya nchi kwa hiyo tunahitaji madaktari ambao wako kwenye vituo hivyo kushirikiana nasi katika kuhakikiasha kwamba swala la tathmini linafanywa kwa haraka na hivyo muhusika anapata fidia stahiki na kwa wakati.” Alifafanua Dkt. Mduma.
Alisema Mfuko utaendelea kufanya kazi zake kwa weledi ndiyo maana unaendelea kuwajengea uwezo wataalamu hao wa afya.
“Tumeandaa miongozo ili kuhakikisha kwamba tathmini zinazotolewa na wataalamu hawa zinakuwa na uhakika, zinaaminika na zinatabirika kwa maana kwamba ziko consistent pale ambapo ukifanyiwa tathmini na mtaalamu A na B matokeo yasitofautiane sana.” Alifafanua.
Dkt. Mduma aliishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu na Serikali kwa ujumla wake kwa jinsi ambavyo imekuwa ikishirikiana na Mfuko katika kuhakikisha unaendelea kutoa huduma zake kwa ufanisi zaidi.
No comments :
Post a Comment