Thursday, December 30, 2021

ASKOFU MKUU MSTAAFU KANISA LA TAG AZIKWA KIJIJINI KWAO VWAWA,MBOZI MKOANI SONGWE

Naibu Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson akitoa heshima zake za mwisho wakati wa ibada ya mazishi ya Askofu Mkuu mstaafu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Dk Ranwell Mwenisongole iliyofanyika Uwanja wa CCM Songwe .Kulia Kwake ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof, Elisante Ole Grabiel.

Askofu Mkuu mstaafu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Dk Ranwell Mwenisongole alifariki Dunia Desemba 25, 2021 katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa Matibabu akiwa na Umri wa miaka 75. Maziko yake yamefanyika kijijini kwao Vwawa wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe.

Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi akishiriki ibada ya mazishi ya Askofu Mkuu Mstaafu  wa Kanisa la TAG Ranwell Mwenisongole, ibada iliyofanyika Uwanja wa CCM Songwe.Waziri Mahundi ametoa pole kwa Kanisa,waumini na mtoto wa marehemu ambaye ni Mbunge wa Mbozi George Mwenisongole.

    

No comments :

Post a Comment