
Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tutuba akizungumza leo Novemba 1,2021 jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari na Waandishi wa habari kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya Fedha na maadhimisho ya wiki ya Huduma za Kifedha Kitaifa inayotarajiwa kuanza Novemba 8-14 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu kwenye maadhimisho hiyo imetajwa kuwa ni ‘Boresha Maisha kupitia Elimu ya Fedha’.
Kamishna Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha Dkt. Charles Mwamwaja akitoa maelezo ya kikao kazi hicho kabla ya kufunguliwa kati ya Wizara ya Fedha na Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali nchini, Kikao hicho pamoja na mambo Kadhaa kinajadili kuhusu Sekta ya Fedha na Maadhimisho ya wiki ya Huduma za Kifedha Kitaifa ambacho kinafanyika kwenye ukumbi wa Kambarage Ofisi ya Hazina jijini Dodoma.Kaimu Kamishna Msaidizi Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Bi. Dionisia Mjema akisikiliza maswali kutoka kwa washiriki wa mkutano huo mara baada ya kuwasilisha mada yake kuhusu Wasilisho la Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha.
Kaimu Kamishna Msaidizi Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Bi. Jannet Hiza akitoa mada kuhusu Programu ya Kutoa Elimu kwa Umma ya Mwaka 2021/22-2025/26.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu Serikali Bw. Emmanuel Tutuba kulia ,Kamishna Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha Dkt. Charles Mwamwaja pamoja na Kamishna Msaidizi Wizara ya Fedha Dionisia Mjema

Afisa Uhusiano, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Zanzibar, Bi. Asha Hussein Saleh (kushoto) na Bw.Salim Kimaro, Afisa Msimamizi Mkuu wa Fedha, Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha

Baadhi ya maafisa habari kutoka taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kweye mkutano huo.


Baadhi ya Wahariri wa Habari wakifuatilia mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye mkutano huo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha Bw. Benny Mwaipaja akitoa ratiba na miongozo mbalimbali katika mkutano huo

No comments :
Post a Comment