Thursday, November 11, 2021

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS ZANZIBAR (FEDHA NA MIPANGO) ATEMBELEA BANDA LA NSSF WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA KITAIFA

 Waziri wa Nchi Afisi ya  Rais, Fedha na Mipango, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Jamal Khamis Ali (kushoto) akizungumza jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam Mhe. Fatma Almasi Nyangassa (wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Masha Mshomba (watatu kulia) na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko huo,  Lulu Mengele (kulia) wakati alipotembelea banda la NSSF wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Novemba 11, 2021. NSSF inaendelea kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba akipata maelezo kutoka kwa Afisa matekelezo mwandamizi Hawa Godigodi, alipotembelea banda la NSSF wakati wa Maonesho  ya Wiki ya Huduma za Fedha kitaifa katika viwanja  vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) Masha Mshomba akielezea huduma mbalimbali zinazotelewa na NSSF katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa. Katika maadhimisho hayo NSSF inatoa elimu kuhusu hifadhi ya jamii, elimu kuhusu umuhimu wakujiwekea akiba, elimu ya  huduma zinazotolewa kwa njia  ya  mtandao ambapo ndio kipaumbele muhimu cha Mfuko pamoja na kueleza fursa za uwekezaji.
Mkurugenzi wa Idara ya Hifadhi ya Jamii, Ofisi ya Waziri Mkuu, Festo Fute (wapili kushoto) akisisitiza jambo alipotembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha kitaifa katika viwanja  vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, kulia ni Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma, Lulu Mengele  pamoja na wafanyakazi wa  NSSF
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mduma (kulia), akipata maelezo mbalimbali kuhusu ushiriki wa NSSF katika  Maonesho ya Wiki ya Huduma za  Fedha kitaifa. Maonesho haya yanaendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa  Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Afisi ya  Rais , Fedha na Mipango, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Jamal K. Ali kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na NSSF wakati wa  Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha kitaifa katika viwanja vya Mnazi mmoja.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko  Taifa wa Hifadhi ya Jamii  (NSSF), Masha Mshomba (wa kwanza mstari wa mbele)  akiwa katika ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam
Waziri wa Nchi, Afisi ya  Rais Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Jamal K. Ali (aliyekaa katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Uendelezaji wa Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha Dkt. Charles Mwamwaja (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Fatma Nyangasa na viongozi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa  wa Hifadhi  ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, akiwa katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa ambapo alipata fursa ya  kutembelea na kupata maelezo katika banda la Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi  (WCF) na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). Mifuko hiyo ipo katika viwanja vya Mnazi mmoja kutoa elimu kuhusu  huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wanachama wao.

No comments :

Post a Comment