Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja (NIC), Bw.Yessaya Mwakifulefule Mkurugenzi wa UDSM Marathon Bi.Lulu Kaaya wakionesha jezi ambayo itatumika katika mbio za UDSM Marathon ambazo zinatarajia kufanyika DISEMBA 4,2021 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja (NIC), Bw.Yessaya Mwakifulefule Mkurugenzi wa UDSM Marathon Bi.Lulu Kaaya wakipongezanawakisaini mkataba wa makubaliano NIC kudhamini mbio za UDSM Marathon ambazo zinatarajia kufanyika Novemba 4,2021 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja (NIC), Bw.Yessaya Mwakifulefule Mkurugenzi wa UDSM Marathon Bi.Lulu Kaaya wakionesha mkataba uliosainiwa NIC kudhamini mbio za UDSM Marathon ambazo zinatarajia kufanyika Novemba 4,2021 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja (NIC), Bw.Yessaya Mwakifulefule Mkurugenzi wa UDSM Marathon Bi.Lulu Kaaya wakipongezana mara baada ya NIC kusaini mkataba wa makubaliano kudhamini mbio za UDSM Marathon ambazo zinatarajia kufanyika Novemba 4,2021 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa UDSM Marathon Bi.Lulu Kaaya akizungumza mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano na NIC kudhamini mbio za UDSM Marathon ambazo zinatarajia kufanyika Novemba 4,2021 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja (NIC), Bw.Yessaya Mwakifulefule akizungumza mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano kudhamini mbio za UDSM Marathon ambazo zinatarajia kufanyika Novemba 4,2021 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) wameingia mkataba wa makubaliano wa kudhamini mbio za UDSM Marathon ambazo zinatarajiwa kutimua vumbi Disemba 04, 2021 kuanzia na kumalizika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja (NIC), Bw.Yessaya Mwakifulefule amesema wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika sekta ya michezo kwa lengo la kukuza vipaji kwa watanzania na pia kujiepusha na magonjwa nyemelezi.
Amesema wanakila sababu ya kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa maana wamekuwa wadau wakubwa kwao katika biashara pia ndio kitivu cha elimu hapa nchini.
"Ni mara yetu ya kwanza kusapoti UDSM Marathon na haitakuwa mara ya mwisho kufanya hivyo, tutaendelea kushirikiana kama ambavyo wamekuwa wadau wakubwa kwetu kwa muda mrefu". Amesema Bw.Mwakifulefule.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa UDSM Marathon Bi.Lulu Kaaya amesema katika mbio hizo wanatarajia kuwepo kwa mgeni rasmi ambaye atakuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete ambaye pia atashiriki kukimbia Kilomita 5.
Amesema mbio hizo zitakuwa na ruti kubwa tatu ambazo ni ruti ya Kilomita 21.1, ruti ya kilomita 10 na ruti ya kilomita 5 ambayo ruti hiyo mgeni rasmi atashiriki
'Lengo kuu la mbiu hizi ni kwaajili ya uchangishaji wa fedha kwaajili ya kuboresha maisha ya wanachuo. Kwasasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kipo katika ujenzi wa kituo cha wanafunzi (Student Center) inayojengwa kwenye Campus ya Mwalimu Nyerere Mlimani Jijini Dar es Salaam ambacho ni mahususi kwa kutoa mazingir mazuri ya mapumziko kwa wanafunzi". Amesema
No comments :
Post a Comment