Thursday, November 18, 2021

TIGO WAZINDUA KAMPENI YA "WAGIFTISHE GIFT JUU YA GIFT

Meneja Mawasiliano kutoka Tigo,Woinde Shisael,akitambalisha, kampeni mpya iitwayo, Wagiftishe, Gift juu ya Gift, Kampeni hii ni kwa ajili ya wateja wapya na wazamani wa mtandao wa Tigo ambapo mteja atakayenunua simu janja ya ITEL T20 Kwa gharama ya shilingi 89,000 kutoka katika maduka ya Tigo nchi nzima watapata intaneti ya BURE GB 72 kwa mwaka mzima na wakati huohuo ataingia kwenye droo ya kushinda simu janja 12 kila siku na pikipiki moja kila wiki kwa kipindi cha wiki sita.,pembeni yake ni mhamasishaji wa kampeni hiyo, kushoto ni Mzee Shayo.

KAMPUNI inayoongoza katika kuhakikisha Mtanzania anaishi Maisha ya Kidigitali hapa nchin, Tigo, imezindua kampeni mpya ya kufunga mwaka inayofahamika kama "WAGIFTISHE GIFT JUU YA GIFT" yenye lengo na dhumuni la kufanya sikukuu za mwisho wa mwaka kuwa za kipekee wa wateja wa Tigo nchi nzima ambapo mteja atapata nafasi ya kushinda simu janja hadi 12 kila siku ndani ya wiki sita.

Kampeni hii ni kwa ajili ya wateja wapya na wazamani wa mtandao wa Tigo ambapo mteja atakayenunua simu janja ya ITEL T20 Kwa gharama ya shilingi 89,000 kutoka katika maduka ya Tigo nchi nzima watapata intaneti ya BURE GB 72 kwa mwaka mzima na wakati huohuo ataingia kwenye droo ya kushinda simu janja 12 kila siku na pikipiki moja kila wiki kwa kipindi cha wiki sita.

Akizungumza katika uzinduzi wa KAMPENI hii Meneja Mawasiliano kutoka Tigo ,Woinde Shisael amesema kuwa "Kampeni hii inalenga kuongeza watumiaji wa simu janja nchini ili kuunga mkono jitihada za serikali katika kukuza teknologia ya habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutoka 45% mwaka 2021 hadi 80% kufikia mwaka 2025 . Lakini pia kama mtandao unaoongoza kwa ubunifu na utoaji wa huduma za Kidigitali nchini kampeni hii itawawezesha wateja wetu kujipatia simu janja mpya na za kisasa alikadharika kuwanunulia ndugu , jamaa na marafiki huku wakijipatia mtandao wenye kasi zaidi wa 4G.

Kwa kipindi chote cha sikukuu za mwisho wa mwaka wateja wa Tigo wamekua wakifurahia ofa kabambe za punguzo la bei za simu pamoja na GIFT kemkem kwa ajili yao na ndugu zao , ambazo tunaamini zinaunganisha familia , Ndugu , jamaa na marafiki pamoja na kudumisha upendo ndo maana tumekua tukiendelea kutoa Ofa hizi kila mwisho wa mwaka ikiwa kama Ishara ya kuwajali na kuwathamini wateja wetu". Alimalizia Bi.Woinde.

Sasa Mteja atakayenunua simu janja ya ITEL T20 kwa ajili yake au familia yake kutoka maduka ya Tigo nchi nzima , atajijengea nafasi ya kushinda moja ya simu janja 504 au moja kati ya pikipiki 6 zitakazotolewa katika KAMPENI hii kwa kipindi cha wiki sita.
Mzee Shayo akizungumza wakati wakutambalisha, kampeni mpya iitwayo, Wagiftishe, Gift juu ya Gift, Kampeni hii ni kwa ajili ya wateja wapya na wazamani wa mtandao wa Tigo ambapo mteja atakayenunua simu janja ya ITEL T20 Kwa gharama ya shilingi 89,000 kutoka katika maduka ya Tigo nchi nzima watapata intaneti ya BURE GB 72 kwa mwaka mzima na wakati huohuo ataingia kwenye droo ya kushinda simu janja 12 kila siku na pikipiki moja kila wiki kwa kipindi cha wiki sita.,pembeni yake ni mhamasishaji wa kampeni hiyo kulia ni Meneja Mawasiliano kutoka Tigo,Woinde Shisael.

No comments :

Post a Comment