Friday, November 12, 2021

TANZANIA YAWASILISHA HOTUBA YAKE MKUTANO MKUU WA 41 UNESCO

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali-Zanzibar Simai Mohammed Said akiwasilisha hotuba katika Mkutano Mkuu wa 41 UNESCO leo Novemba 12,2021.
Balozi na Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa UNESCO Samwel Shelukindo,(kulia) na Profesa Hamis Malebo, Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO(kushoto)


Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Simai Mohammed Said, kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewasilisha hotuba kwenye Mkutano Mkuu wa 41 wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), unaoendelea jijini Paris, Ufaransa.

Akiwasilisha hotuba hiyo leo Novemba 12,2021 Waziri alianza hotuba yake kwa kufahamisha msimamo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kuendelea kuunga mkono kazi za UNESCO kama njia ya kuimarisha diplomasia majumui (Multilateral Diplomacy).

Waziri alieleza kuhusu juhudi za nchi katika kuhakikisha upatikanaji wa elimu kwa misingi ya usawa baada ya kutokea Janga la UVIKO-19. Vilevile Waziri amepongeza jitihada za UNESCO katika kuwezesha Nchi Wanachama kuimarisha ufundishaji wa masomo ya sayansi na kueleza juhudi za nchi katika kuimarisha Sekta ya Ubunifu.

Ambayo imeajiri Watanzania wengi, idadi kubwa ikiwa ni vijana.Pia Waziri alithibitisha nia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea na utekelezaji wa majukumu ya UNESCO sambamba na Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030.

No comments :

Post a Comment