Monday, November 15, 2021

JAJI MKUU AFUANGUA MAFUNZO KWA MAJAJI WAPYA WA MAHAKAMA

Mhe. Dkt Paul F. Kihwelo Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama na Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania akifungua mafunzo kwa wawezeshaji wa mafunzo ya haki za watoto mafunzo yatafanyika katika ukumbi yanayofanyika katika ukumbi wa St. Gasper jijini Dodoma.
Bi. Victoria Mgonela Mwakilishi wa UNICEF akitoa salamu kutoka Shirika la UNICEF nchini Tanzania kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika katika ukumbi wa St. Gasper jijini Dodoma
Picha ya pamoja ya majaji wanaoshiriki katika mafunzo kwa wawezeshaji wa mafunzo ya haki za watoto. Mafunzo haya yanafanyika katika ukumbi wa St. Gasper jijini Dodoma.
Picha ya pamoja ya majaji wanaoshiriki katika mafunzo kwa wawezeshaji wa mafunzo ya haki za watoto na washiriki wengine waliohudhuria katika mafunzo hayo yanayofanyika katika ukumbi yanayofanyika katika ukumbi wa St. Gasper jijini Dodoma.
 Baadhi ya Washiriki wa mafunzo kwa wawezeshaji wa mafunzo ya haki za watoto wakiwa wanasikiliza mada zinazoendelea katika mafunzo hayo kutoka kwa muwezeshaji Mhe. Sophia Wambura Jaji Mstaafu (hayupo pichani).
JAJI Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amefungua rasmi Mafunzo elekezi ya kwanza kufanyika kwa Majaji wapya wa Mahakama ya Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu Zanzibar walioteuliwa tarehe Mei 11, 2021 na kuapishwa tarehe Mei 17, 2021 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Sululu Hassan.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa jumla ya Majaji 31 ambapo 7 ni Majaji wa Mahakama ya Rufani, 21 Majaji wa Mahakama Kuu pamoja na Majaji 3 wa Mahakama Kuu ya Zanzibar. Mafunzo hayo ambayo yameratibiwa na kufanywa na Mahakama ya Tanzania kupitia na kushirikiana na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) Mhe. Jaji Prof. Juma alisema kuwa, mafunzo endelevu kwa Majaji yana umuhimu wa kipekee na ni moja ya kigezo cha msingi katika kuboresha utoaji wa haki.

Akiongea katika uzinduzi wa Mafunzo kwa Majaji hao Mhe. Jaji Prof. Juma aliwapongeza Majaji kwa kukubali kwenye nafasi ya Ujaji kwani kanuni na maadili ya kazi hiyo ni kujinyima sehemu kubwa ya uhuru wa maisha yao ya binafsi kwenye nyendo zao za kila siku.

Akinukuu maneno ya Jaji Mstaafu J.K Mathur aliyekuwa anahudumu Mahakama Kuu ya Calcutta chini India kwenye maandiko yake , ” Mhe. Jaji Prof. Juma alisema kuwa, andiko hilo huwakumbusha mambo makuu matatu katika mafunzo ya Maafisa wa Mahakama ambayo ni Maarifa, Ujuzi na Mtazamo.

“Mambo hayo yanatakiwa kuzingatiwa katika utendaji kazi wa Majaji wa Mahakama ya Rufani na Majaji wa Mahakama Kuu,” alieleza Mhe.Prof. Juma.

Akinukuu maneno ya Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chance Othmna alipokuwa anatoa mada mwaka 2016 kwenye semina ya Uongozi kwa waheshimiwa Majaji kwa kuwauliza “Je Mnajitambua kama Majaji nyie ni viongzo” alisema Mhe. Prof Juma. Akielezea hilo aliwakumbusha kuwa kila mmoja wenu ni kiongozi hivyo basi wananchi wa Tanzania wanamatarajio makubwa kwenu katika sekta ya sekta ya utoaji haki.

Mhe. Dkt Eliezer Mbuki Feleshi, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania akitoa maelezo ya utangulizi alisema kuwa, kwa kutoa shukurani nyingi kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuona uhitaji mkubwa wa rasilimali watu kwenye kada ya Majaji na kufanya teuzi hizo.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo Mhe. Dkt. Fauz Twaib, Jaji wa Mahakama Kuu (Mstaafu) Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi na Mkurugezi wa Mafunzo ya Majaji hao akitoa neno la shukrani kwa hadhara hiyo, Mhe. Gerald Ndika Jaji wa Mahakama ya Rufani alimshukuru Jaji Mkuu kwa busara zake na kukiamini Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kuwa kina uwezo wa kuandaa, kufanya na kutoa mafunzo yenye ubora unahitajika kwa Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama kuu. 

“Sina shaka kwamba hotuba hiyo imetutia hamasa na imetuweka katika hatu nzuri ya kuandaa na kuendesha mafunzo elekezi” Pia aliishukuru zaidi Menejimenti ya Chuo kwa kufikiria kwa mapana Zaidi kwa kuandaa programu ya siku saba kwa kwa Majaji wa Mahakama ya Rufani na siku 10 kwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Zanzibar.

Hii ni mara ya pili kwa Majaji Wapya wa Mahakama ya Rufani kupewa mafunzo elekezi na ni mara ya sita kwa Majaji wa Mahakama Kuu Tanzania kupewa mafunzo elekezi tangia utaratibu huu uanze mwaka 2014. Mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika katika makundi mawili yanayojumuisha Majaji 7 wa Mahakama ya Rufani walioapishwa hivi karibuni wakati kundi la pili linajumuisha Majaji 21 wa Mahakama Kuu ya Tanzania walioapishwa hivi karibuni pamoja na Majaji 3 wa Mahakama Kuu Zanzibar ambao nao ni Majaji Wapya.

No comments :

Post a Comment