Friday, November 12, 2021

DART Kunufaika Na KAIZEN

Mwakilishi wa Katibu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Tawala za Mitaa(Tamisemi) Zubeda Masoud akizungumza wakati uzinduzi wa Mafunzo ya KAIZEN  kwa Watendaji wa DART na Wadau Wengine uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala ya Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Dk.Edwin Mhede akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana mafunzo ya KAIZEN Wakala wa Mabasi  hayo.
Mkurugezi wa Maendeleo ya Viwanda wa Wizara ya Viwanda na Biashara Lugano  Wilson akitoa faida akizungumza faida KAIZEN  kwa DART.
Mwakilishi Mwandamizi wa JICA nchini Tanzania Matsuyama Satoru akizungumza kuhusiana na mafunzo KAIZEN



Picha mbalimbali za makundi katika semina hiyo KAIZEN

*Dk.Mhede abiria hatakiwi kusubiri kwa muda mrefu

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV 
WAKALA ya Mabasi Yaendayo Haraka (DART) umepata mafunzo ya Shirika la Maendeleo ya Japan JICA kupitia mradi wake urahishaji wa kiutendaji KAIZEN utaofanya DART kwenda kwa kasi katika ukuaji wa uchumi katika usafirishaji usiochelewa kwa Jiji Dar es Salaam.

Akizungumza katika ufunguaji semina kwa watendaji wa DART pamoja na wadau wanaofanya kazi moja kwa moja Wakala huo Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (TAMISEMI), Zubeda Masoud amesema mafunzo ya KAIZEN yatumike katika kutatua baadhi ya changamoto na kuleta matokeo chanya ya kiutendaji kwa wakala wa mabasi katika kuhudumia wananchi kwa kufanya ukuaji wa uchumi kwa haraka.

Amesema Japan wamekuwa wadau wakubwa katika maendeleo ya ujenzi wa miundombinu hivyo kuwa na programu ya mafunzo yatasaidia utendaji wa wakala kwenda kasi zaidi kuliko ilivyosasa.

Masoud amesema mafunzo hayo ni matarajio yao yataleta tija kwa wakala katika kuweka mazingira rafiki na kuokoa muda katika utoaji huduma za usafiri kwa jiji Dar es Salaam.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa DART, Edwin Mhede amesema kuwa kupitia Kaizen watakwenda kutekeleza kuhakikisha wananchi hawapotezi muda wao katika kusubiri usafiri ambapo kiuchumi itakuwa na faida sana.

Dk.Mhede amesema katika kwenda kasi wafanyakazi kuacha kupoteza muda kutokana na masuala mengi kuweka katika mfumo wa kaizen ambao Japan uliwapa matokeo chanya zaidi.

Amesema pamoja na kuweza kupata matokeo chanya wataboresha tija mahala pakazi na wadau wote kuacha kupoteza muda wa kazi.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda, Lugano Wilson amaesema KAIZEN imeweza kubadili Wizara ya Viwanda kwa kuweka vitu katika mifumo na kurahisisha utendaji wake.

Amesema kuwa kama sehemu ya watu kunufaika na kaizen ambapo DART watasaidia katika usafirishaji wa wananchi na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Mwakilishi Mwandamizi wa JICA Nchini Tanzania Matsuyama Satoru amesema kuwa KAIZEN itawapa matokeo chanya katika upangaji wa mifumo.

No comments :

Post a Comment