Sunday, November 14, 2021

BoT YAPONGEZWA KWA UTHABITI WA UCHUMI NA SEKTA YA FEDHA NCHINI

Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Paschal Katambi Patrobas, akizungumza alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha katika viwanja vya Mnazi Mmoja, ambapo ameipongeza BoT kwa kazi inayofanya kuhakikisha ukuaji na uthabiti wa uchumi wetu na sekta ya fedha nchini. Kulia ni Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, Bi. Victoria Msina.

Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, Bi. Victoria Msina, akimkabidhi zawadi Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Paschal Katambi Patrobas, alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 08 – 14 Novemba 2021.

Mchambuzi wa Masuala ya Fedha BoT, Bi. Gloria Chellunga, akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha kuhusu namna ya kuwekeza katika Dhamana za serikali za muda mrefu (Treasury Bonds) na muda mfupi (Treasury Bills).

Afisa Benki BoT, Bw. Jovitha Kalokola, akitoa elimu kwa mwananchi kuhusu namna ya kutambua alama za usalama zilizopo katika noti zetu.

Afisa Rasilimali Watu Mwandamizi kutoka Bodi ya Bima ya Amana (DIB), Bi. Joyce Shala,  akifafanua jambo kwa mwananchi alietembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania kuhusu namna Bodi hio inavyofanya kazi.

Mchumi kutoka BoT, Bw. Lucas Magazi, akitoa elimu kuhusu usimamizi wa fedha binafsi kwa mwananchi alietembelea  banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 08 – 14 Novemba 2021.

Wafanyakazi wa Jiji la Ilala wakizungumza na Mkaguzi wa Mabenki BoT, Bw. Michael Tumaini, kuhusu usimamizi wa watoa huduma ndogo za fedha walipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 08 – 14 Novemba 2021.

 

No comments :

Post a Comment