Monday, October 4, 2021

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA BODI YA WADHAMINI YA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF)

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Joachim Mhagama (MB)  (kulia) akimkabidhi mkoba wenye Nyaraka mbalimbali, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF). Bw. Emmanuel Humba, mara baada ya kuzindua Bodi hiyo mkoani Morogoro Oktoba 4, 2021
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Joachim Mhagama
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Emmanuael Humba 
Mkurugenzi Mkuu wa WCF Dkt. John Mduma, akitoa hotuba yake
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Joachim Mhagama akimkabidhi nyaraka, Mjumbe wa Bodi Bi. Julian C.N. Mpanduji
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Joachim Mhagama akimkabidhi nyaraka, Mjumbe wa Bodi Bi. Rehema Rashid Ludanga
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Joachim Mhagama akimkabidhi nyaraka, Mjumbe wa Bodi Bw. Abdulaziz Alladin Shambe
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Joachim Mhagama akimkabidhi nyaraka, Mjumbe wa Bodi Bw. Perfect Raphael Kilenzi
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Joachim Mhagama akimkabidhi nyaraka, Mjumbe wa Bodi 
Bw. Raymond Kaseko
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Joachim Mhagama akimkabidhi nyaraka, Mjumbe wa Bodi Bw.Ibrahim Barnabas Mahuni
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Joachim Mhagama akimkabidhi nyaraka, Mjumbe wa Bodi Bw.Felix Kagisa Rugarabamu.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Joachim Mhagama (MB), amezindua Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) leo Tarehe 4/10/2021 Mjini Morogoro.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Jenista Mhagama amempongeza Mwenyekiti Mpya wa Bodi hiyo Bw. Emmanuel Humba kwa kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo na pia amewapongeza Wajumbe wa Bodi aliowateua na kuwataka waende kuusimamia Mfuko kwa kushirikiana na Menejimenti ili kufikia matarajio ya Serikali.

Wajumbe wapya wa Bodi walioteuliwa na Mhe. Waziri Jenista Mhagama ni pamoja na Ornorius John Njole, Perfect Raphael Kilenzi, Ibrahim Barnabas Mahuni, Abdulaziz Alladin Shambe, Rifai A. Mkumba, Julian C.N. Mpanduji, Rehema Rashid Ludanga na Felix Kagisa Rugarabamu.

“Naomba mfahamu kwamba tunapofanya maamuzi haya mazito ya kuwateua tunajua Bodi ni chombo cha Juu cha Uendeshaji wa kila siku wa Taasisi husika, Sisi wote hata Mkurugenzi wa Mfuko, Wafanyakazi wenyewe, Waajiri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Rais, ni kama vile tumekasimu madaraka yetu sisi wote kwa mujibu wa Sheria na kukasimu kwako Mwenyekiti na Bodi.” Alisema Mhe. Waziri.

Mhe. Jenista Mhagama amewataka wajumbe hao kuyaelewa vema majukumu yao kama yalivyoanishwa isheria katika kifungu cha 13, 14, 15 na 16, na sehemu ya majukumu hayo ni pamoja na kusimamia maslahi ya wafanyakazi yanayotokana na kuanzishwa kwa sharia ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.

 “ Kumekuwa na Mafanikio makubwa ya Mfuko katika kipindi hiki cha miaka sita na mnatakiwa kuyalinda kwa wivu na kwa nguvu zenu zote.” Alifafanua na kutoa mfano………katika kipindi ambacho bodi haikuwepo, thamani ya Mfuko imekuwa hadi kufikia shilingi za Kitanzania bilioni 445.49 kutoka thamani ya Mfuko mwaka 2016/2017 shilingi bilioni 112.83,  huu ni ukuaji mkubwa sana na tunaona kuna kazi kubwa imefanyika, lindeni mafanikio haya.” Alisisitiza.

 Akizungumzia ulipaji wa Mafao, Mhe. Waziri Mhagama alisema kufikia 2020/2021 Mfuko ulilipa Mafao ya Wafanyakazi waliopata ajali kazini shilingi bilioni 12.43 ikilinganishwa na mwaka 2017 ambapo zililipwa shilingi bilioni 1.55 tu.

Waziri aliitaka Bodi kuhakikisha Mafanikio yaliyofikiwa na Mfuko hadi sasa yanasimamiwa na kubuni mikakati mipya ya kuhakikisha Mfuko unatoa huduma kwa walengwa kwa wakati na uhakika kwa kufanya uwekezaji ili fedha za waajiri zisikae tu.

Aidha aliwaasa Wajumbe wa Bodi kuelewa vema lengo la uwepo wa Mfuko ambapo ni kuhakikisha Wafanyakazi wanaoumia, Kuugua ama Kufariki kutokana na Kazi zao kwa mujibu wa Mikataba ya Ajira zao basi Serikali kupitia WCF iwalipe fidia au iwatibu na wakipona warejee kazini kuendelea na majukumu yao.

“Kubwa ni kuendelea kuimarisha Mifumo na utoaji elimu kwa walengwa ili Waajiri na Wafanyakazi waujue Mfuko na majukumu yake……Sasa hivi tunasema tuko kwenye uchumi wa Viwanda, viashiria vingi vya uwepo wa ajali kazini na eneo mojawapo ni kwenye sekta ya Viwanda na Usafirishaji kwahiyo lazima Bodi ihakikishe muelekeo unajikita kwenye utoaji elimu kwa wadau mbalimbali.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Emmanuael Humba alimuhakikishia Mheshimiwa Waziri Mhagama kuwa watahakikisha Mfuko unaendelea kutekeleza majukumu yake kulingana na malengo ya Mfuko.

“Mashirika mengi yanakufa kutokana na kujisahau kwa waliopewa dhamana ya kusimamiwa mashirika haya, sisi ni wadhamini tu, na kwahiyo udhamini wetu lazima tuulinde kwa hali na mali kwa kutenda haki.” Alisema Bw. Humba.

Bw. Humba alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini kuongoza Bodi hiyo na kutoa hakikisho ya kufanya kazi kwa uwezo wake wote.

“Naomba wajumbe wenzangu tuutendee haki uaminifu ambao Mheshimiwa Rais na Mheshimiwa Rais wametupatia kwa kufanya kazi kwa Weledi na bidii kwa hiyo nawaombeni tutende haki.” Alibainisha.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa WCF Dkt. John Mduma alimpongeza Mwenyekiti wa Bodi Bw. Emmanuel Humba kwa kuaminiwa kupewa dhamana hiyo kwa kipindi cha pili lakini pia kuwapongeza wajumbe wote walioteuliwa na Mheshimiwa Waziri katika kuendesha gurudumu la Mfuko.

Alimpongeza Mhe. Waziri kwa kuteua wajumbe kwa kuzingatia kubakia kumbukumbu ya Taasisi kwa kuwabakisha wachache waliokuwepo na kuteua wengine wapya hali itakayosaidia kuufikisha Mfuko mahala panapostahili.


No comments :

Post a Comment