Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma leo.
SERIKALI imetoa maagizo 11 kwa waajiri wa umma wote nchini kufuatia kubainika kwa changamoto mbalimbali kwa watumishi wa umma ikiwemo kanuni na taratibu za kiutumishi, Maafisa mipango kutosimamia miradi ya kimkakati ipasavyo, upungufu wa watumishi pamoja na watumishi kutopandishwa madaraja.
Maagizo hayo yametolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala, Mohamed Mchengerwa wakati alipokua akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.
Waziri Mchengerwa ameyataja maagizo hayo kuwa ni pamoja na waajiri kuendelea kushughulikia watumishi wenye sifa za kupandishwa cheo kwa kuwatengea bajeti katika mwaka wa fedha ujao, kushughulikia malipo ya stahiki mbalimbali za watumishi

No comments :
Post a Comment