Na Mwandishi Wetu, Pwani
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA),imeteketeza hekari moja ya shamba lenye mimea ya bangi katika kitongoji cha
Sambamba na uteketezaji huo, Mamlaka imewakamata watu wawili ambao ni wamiliki wa shamba hilo.Watu waliokamatwa ni Khamis Mohamed Tengeneza (59) kabila mzaramo na Abdallah Mohamed Hemba (48) kabila mzaramo wote wakazi wa Kiremeta.
Taarifa iliyotolewa leo Oktoba 2,2021 kwa vyombo vya habari na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Mamlaka hiyo Florence Khambi amesema shamba hilo limetekezwa Oktoba 1 mwaka huu sambamba na kukamatwa watu hao.
"Watuhumiwa wametenda kosa hilo kinyume cha kifungu cha 11(1) (a) cha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Namba 5 ya mwaka 2015 kama ilivyorejewa mwaka 2019,"amesema.
Amefafanua mpaka sasa watuhumiwa wameshikiliwa na wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani taratibu za kisheria zitakapokamilika.
No comments :
Post a Comment