Friday, October 22, 2021

Tanzania Yaendelea Kushirikiana Na Mataifa Duniani Katika Kupambana Na Dawa Za Kulevya

Na Mwandishi Wetu, Vienna Nchini Austria

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Gerald Kusaya akiambatana na maafisa wengine ameiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa 64 wa Majadiliano ya Kamisheni ya Kimataifa ya Kudhibiti Dawa za Kulevya Duniani ulioanza Oktoba 18 - 21 Mwaka huu Jijini Vienna Nchini Austria.

Mkutano huo wenye lengo la kubadilishana uzoefu, kuimarisha ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa pamoja na kutatua changamoto zinazojitokeza katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Pia,  Mkutano huo  ulijadili namna bora ya kupambana na tatizo la dawa za kulevya na makosa mengine ya uhalifu wa kupangwa ikiwepo ya Ugaidi, Utakatishaji fedha, Usafirishaji haramu wa Binadamu na Uhalifu wa kimtandao na kuimarisha ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa pamoja nakutatua changamoto zinazojitokeza katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya Duniani

No comments :

Post a Comment