Tuesday, October 19, 2021

Serikali Yaombwa Kuongeza Walimu Maalumu Watakao Wafundisha Lugha Za Alama Watoto Wenye Umri Wa Kwenda Shule Za Awali

 Raisa Said,Tanga

Serikali imeombwa kuangalia uwezekano wa kuongeza Walimu wenye elimu Maalumu na Vitendea kazi vitakavyo wasaidia watoto wenye ulemavu na wenye  umri chini ya miaka mitano ambao wanakumbana na changamoto ya lugha ya alama.

Akizungumza na Mwandishi  wa habari hizi  Afisa Utetezi kutoka kituo cha Watoto wenye ulemavu kilichopo Jijini Tanga (YDCP)  Prisca Mwakasendile Alisema  kuwa uhitaji wa Walimu na Vitendea kazi katika vituo vya Watoto wenye ulemavu na Shule zenye madarasa ya watoto hao ni mkubwa.

Mwakasindile alisema kuwa lugha ya alama ni lugha Mama na ambayo ni sehemu ya maisha kwa Watoto wenye ulemavu wa kusikia (viziwi)  hivyo walimu maalumu wakiongezeka wanaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa  wawapo shuleni hata mtaani kwenye maisha ya Kila siku.

Alisisitiza  changamoto  wanayokumbana nayo kwa watoto hususani wenye umri mdogo chini ya miaka mitano ambao wengi wao ni darasa la awali hawajui Lugha za alama ambazo zinatambulika  walimu na Wazazi jambo ambalo linawachukua muda katika ufundishaji

Aliongeza kwa kuiomba serikali ijenge vitengo vya Watoto hao huku akisisitiza walimu wasiwachanganye Watoto hao darasa moja na Watoto wasiokuwa na ulemavu ili iwe rahisi katika ufundishaji na uelewa kwa mtoto husika.

Alitumia  fursa hiyo kuwataka Wazazi na walezi waone umhimu wa kuwapeleka watoto wao shule ili wapatiwa elimu nakuondokana na dhana potofu ya kuwaficha majumbani watoto wenye ulemavu kwani kila mtoto ana haki ya kupata elimu.

Hata hivyo alisisitiza Suala la Malezi na makuzi ni jukumu la wazazi wote na jamii kwa ujumla tuungane kwa pamoja kuhakikisha watoto ambao ni tunu ya taiifa wanapatiwa haki zao za msingi.

Kwa Upande wake Mzazi Mwenye mtoto Mwenye ulemavu kutoka kisosora  alisema Kuna wakati anapata changamoto kumuelewa mtoto wake anazungumza nini hasa pale anapokiwa  na uhitaji was kitu


No comments :

Post a Comment