Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi akizungumza na wanachama wa Chama Cha Wataalamu wa Udhibiti wa Ufisadi na Ubadhilifu (ACFE) wakati akizindua mkutano wao jijini Arusha leo.
Rais wa Chama Cha Wataalamu wa Udhibiti wa Ufisadi na Ubadhilifu ACFE, Stella Cosmas akizungumza katika mkutano wa kila mwaka wa chama hicho leo jijini Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela akizungumza katika mkutano wa Chama cha Wataalamu wa Udhibiti wa Ufisadi na Ubadhilifu ACFE uliofanyika jijini Arusha leo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali na washiriki wa mkutano wa kila mwaka wa ACFE uliofanyika jijini Arusha leo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi akizungumza katika uzinduzi wa mkutano wa kila mwaka wa ACFE jijini Arusha.
Rais wa Chama Cha Wataalamu wa Udhibiti wa Ufisadi na Ubadhilifu ACFE, Stella Cosmas akizungumza katika mkutano wa kila mwaka wa chama hicho leo jijini Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela akizungumza katika mkutano wa Chama cha Wataalamu wa Udhibiti wa Ufisadi na Ubadhilifu ACFE uliofanyika jijini Arusha leo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali na washiriki wa mkutano wa kila mwaka wa ACFE uliofanyika jijini Arusha leo.
Charles James, Michuzi TV
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi ametoa wito kwa Taasisi za Serikali na binafsi zikiwemo Taasisi za Kifedha kujiunga na Chama Cha Wataalamu wa Udhibiti wa
Ndejembi ametoa mwito huo leo jijini Arusha wakati akizindua mkutano mkuu wa kila mwaka wa Chama hicho ambapo wanachama wake hukutana na kubadilishana uzoefu mbalimbali unaolenga mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi na ubadhilifu.
Amesema mchango wa Asasi kama ACFE katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi ni mkubwa ambapo anaamini kuwa kwa ushirikiano wa pamoja baina yao kama Serikali na Asasi hizo utachochea kuimarisha mapambano dhidi ya vitendo hivyo na hatua iliyopigwa na Serikali kwenye kukabiliana navyo itasonga mbele zaidi.
"Kama mnavyofahamu tunatambulika duniani kote na taasisi mbalimbali kama vile Transparency International kuwa Tanzania ni miongoni mwa Nchi zinazofanya vizuri zaidi katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi na yote hayo ni kutokana na chombo imara tulichonacho cha TAKUKURU lakini sasa kwa kushirikiana na wenzetu hawa wa ACFE tutasonga mbele zaidi na kufikia hata 50 Bora ya Nchi zinazofanya vizuri duniani kwenye mapambano ya ufisadi.
Niwapongeze viongozi wa ACFE hii lakini zaidi nitoe wito kwa Taasisi zingine kujiunga nao kwa pamoja kwani kuna mambo mengi watanufaika nayo na sisi kama Serikali tutaendelea kushirikiana nao," Amesema Naibu Waziri Ndejembi.
Kwa upande wake Rais wa ACFE hiyo, Stella Cosmas amesema Chama hicho kina wanachama 300 hadi sasa waliojiunga kutoka Taasisi za Serikali, Binafsi na Mashirika ya Kiraia (AZAKI) ambapo asilimia 75 ya wanachama wake wanatoka Taasisi za Kiserikali ikiwemo TAKUKURU, Jeshi la Polisi, TRA, PSSSF, NSSF, NHIF, TANESCO, ATCL, CRDB, NMB, BOT, TMDA, SUMA JKT, LATRA, TARURA na nyinginezo.
Amesmaa chama hicho kinafanya kazi na taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi ka kuwajengea uwezo, kutoa elimu bure ya ufahamu juu ya vitendo vya ubadhilifu kwa kuwafahamisha viashiria mbalimbali vya kuzuia kabla ubadhilifu haujatokea.
" Kila mwaka tunafanya mkutano kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na kukuza umoja wetu, mwaka huu mada kuu ni Mapambano dhidi ya ufisad, rushwa na ubadhilifu katika kujenga Taifa lenye uchumi imara na kauli mbiu yetu ni Tanzania bila ufisadi inawezekana," Amesema Stella
No comments :
Post a Comment