Friday, September 17, 2021

TAWA YASHIRIKI MAONESHO YA UTALII JIJINI ARUSHA.

makuu ya Taasisi hiyo ukiongozwa na Mkuu wa kitengo cha habari na Mahusiano Bw.Twaha Twaibu.





 
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ni Moja ya Taasisi zinazoshiriki maonesho ya utalii yanayofanyika katika viwanja vya michezo vya Kisongo(UWC) Jijini Arusha kwa lengo la kutangaza vivutio vinavyosimamiwa na Mamlaka hiyo.

Mkuu wa kitengo cha habari na Mahusiano wa TAWA Bw.Twaha Twaibu Amesema maonesho hayo ya siku mbili yataleta tija kubwa Sana kwa mamlaka hiyo kwani,kutawapa fulsa ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya Utalii pamoja na kujitangaza.

Moja ya vivutio vinavyosimamiwa na Mamlaka hiyo ni mapori ya Akiba ikiwemo pori Pande lilikopo Jijini Dar Es salaam pamoja Pori la Akiba la Rukwa ambalo lina kivituo kikubwa Cha maporomoko ya Maji ya ndido yanayowafanya watalii wengi kupenda kutembelea Pori Hilo.

Pia mamlaka hiyo inasimamia Maeneo ya Urithi wa Dunia ya KILWA KISIWANI na SONGO MNARA pamoja na pori la Akiba Maswa.Maonesho haya yameanza leo tarehe 17 hadi 18 Septemba,2021 huku TAWA ikiwakirishwan ujumbe kutoka makao makuu ya Taasisi hiyo ukiongozwa na Mkuu wa kitengo cha habari na Mahusiano Bw.Twaha Twaibu.


No comments :

Post a Comment