Mratibu wa mradi wa ushirikishwaji wanawake kushika nafasi za uongozi Salma Amiri Lusangi akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani.
Mkufunzi wa maswala ya habari Zanzibar Dkt,Abuubakari Rajab akiwasilisha ripoti juu ya uwakilishi wa habari za wanawake katika vyombo mbali mbali.
Mwandishi wa habari kutoka shirikia la magazeti ya Serikali Zanzibaer Mwinyimvua Nzukwi kichangia ripoti hio mara baada ya kuwasilishwa.
Na Muhammed Khamis,TAMWA-ZNZ
Mkurugenzi wa Chama cha Waaandishi wa habari Wanawake TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa amesema katika jitihada za kuwaunga mkono wanawake kushika nafasi mbalimbali za uongozi ambapo vyombo vya habari vinawajibu wa
kutoa kipao mbele habari zinazowahusu wanawake viongozi na wale wote ambao wanahitaji kupaziwa sauti zao kwa lengo la kuleta mabadiliko katika jamii.Dkt,Mzuri aliyasema hayo huko Tunguu Wilaya ya kati Unguja katika ofisi za Chama hicho kufuatia uzinduzi wa ripoti ndogo ambayo inatazama kwanamna gani vyombo vya habri vinawaandika ama kuwaripoti wanawake viongozi katika habari za kila siku visiwani hapa.
Alisema kwa kuwa vyombo vya habari vinanafasi kubwa ya kufanya mabadiliko wakati huu ikiwa ni ikiwemo kuandika na kuripoti matukio mbali mbali yanayofanywa na wanawake viongozi Serikali n ahata wasiokua viongozi ndani ya Serikali.
Alisema vyombo vya habari kupitia mkakati maalumu wanawake kuwaandaa wanawake kushika nafasi za uongozi kupitia vipindi vyao vya kila siku kwani wanawake ni watu wanaoitaji motisha.
Alieleza kuwa kikawaida wanawake wengi wamekua wakishindwa kusika nafasi za uongozi kutokana na kukosa maandalizi bora ya kutaka kushika nafasi hizo badala yake wengi wao huamua kujitokeza kugombea nafasi hizo bila kukosa maandalizi mazuri ya awali.
Akiendelea kufafanua zaidi Mkurugenzi huyo alimtolea mfano Rais Samia Suluhu na kueleza kuwa ni mtu aliepitia hatia hatua mbali mbali hadi kufika kuwa Rais na niwazi kwamba ni miongoni mwa wanawake walioandaliwa na kujitengeneza vyema kushika nafasi tofauti mpaka kuwa Raisi.
Sambamba na hayo alisema ili kutimiza malengo hayo vyombo vya habari havina budi kujitoa na kutengeneza kampeni maalumu ya kuwainua wanawake visiwani hapa.
Akiwasilisha ripoti hio mkufunzi wa maswala ya habari Dkt,Abuubakar Rajab alisema kupitia utafiti wake wa vyombo mbali mbali vya habari vinavyofanya kazi visiwani hapa na Tanzania kwa ujumla bado vimekua vikitoa nafasi ndogo sana kwa viongozi wanawake.
Alisema imekua kawaida kutoona habari ianyomuhusu mwanamke kupewa kipao mbele kwenye magazeti au ata redio badala yake wengi wao wanaamini kuwa wanaume ndio wanaopaswa kupewa kipao mbele kila leo.
Akifafanua kuhusu hali hio alisema wahariri wa vyombo vya habari hawana budi kuziona changamoto hizo na kuzifanyia kazi wakijua kuwa kila mtu ana haki sawa na anapaswa kupewa haki yake.
Akizungumza mara baada ya kuwasilishwa kwa ripoti hio Mhariri msaidizi wa shiririka la magazeti ya Serikali Zanzibar Juma Khamis alisema utafiti huo umewafungua na kuona namna gani wamekua wakishindwa kuwatendea haki ipasavyo wanawake kupitia vyombo vyao .
Pamoja na hayo alieleza kuwa watahakikisha wanaweka mkakati maalumu kama wahariri kutoa nafasi zaidi kwa wanawake viongozi na wenye nia ya kutaka kuleta mabadiliko katika jamii mbali mbali.
Kwa upande wake mratibu wa mradi wa ushirikishwaji wanawake katika uongozi kutoka TAMWA-ZNZ Salma Amir Lusangi alisema mradi huo wa miaka mine unalenga kuwawezesha wanawake elfu sita kutoka wilaya 11 za Unguja na Pemba.
Alisema anaamini elimu watakayopatiwa wanufaika wa mradi huo italeta tija hatimae wanawake wengi wataweza kushika nafasi mbali mbali za uongozi iwe kwenye jamii zao au hata za kisiasa.
Mradi wa ushirikishwaji wanawake katika nafasi za uongozi unatekelezwa na TAMWA-ZNZ chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Norway Nchini Tanzania.
No comments :
Post a Comment