Thursday, September 2, 2021

TAMNOA Yapongeza Uamuzi Wa Serikali Kupunguza Na Tozo Za Miamala


Pamoja a hayo, tunaipongeza serikali kwa kupunguza 30 asilimia na kutoweka miamala ya bei ya chini katika utekelezaji wa agizo hili. 

Tunatumai hii pamoja na upunguzaji wa 10 asilimia ya ada za miamala kwenye miamala inayofanyika baina ya wateja wa makampuni tofauti zitarudisha wateja ambao waliacha kufanya miamala tangu kuanza kwa utekelezaji wa agizo hili.

Katika enzi hii ya mapinduzi ya nne ya viwanda, sekta inayostawi ya mawasiliano ina jukumu muhimu la kuwezesha sekta zingine kama teknolojia ya kilimo (Agritech), huduma ya matibabu kwa video (telemedicine) na malipo ya serikali na huduma, nikitaja hayo machache, ili kuendelea kuchangia ukuaji wa Taifa. Mpaka  wakati huu, wanachama wa TAMNOA wamejitolea kuendelea kuwekeza katika uvumbuzi mpya, lakini ili kuwezesha hili, lazima tuendelee kubaki na faida.

Kwa hiyo, kwa muda wa kati na mrefu ujao, bado ni muhimu kwa tasnia kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kushirikishana maarifa na njia bora zaidi za jinsi ya kupata majukwaa ya kidijitali yatakayowezesha ukusanyaji wa kodi kwa ukaribu na mamlaka husika na wadau wengine ili kuhakikisha kunakuwa na usawa latika kutimiza matazamio ya jamii yetu.

-Hisham Hendi, Mwenyekiti- TAMNOA

No comments :

Post a Comment