Wednesday, September 1, 2021

NIC Yatoa Msaada Wa Sh. Milioni 26 Kwa Ajili Ya Ukarabati Wa Mabweni Shule Ya Sekondari Jitegemee

Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Isaya Mwakifulefule (mwenye tai),akimkabidhi mfano wa mfuko mmoja wa saruji  Mkuu wa Shule ya Sekondari Jitegemee Kanali Robert Kessy katika hafla iliyofanyika Shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Isaya Mwakifulefule (mwenye tai),akimkabidhi mfano bati moja Mkuu wa Shule ya Sekondari Jitegemee Kanali Robert Kessy katika hafla iliyofanyika Shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Jitegemee Kanali Robert Kessy akizungumza kuhusiana na msaada uliotolewa na NIC kwa ajili ya ukarabati wa mabweni katika Shule hiyo hafla iliyofanyika Shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Isaya Mwakifulefule akizungumza wakati hafla ya Kukabidhi vifaa vya ukarabati wa mabweni katika Shule ya Sekondari Jitegemee iliyofanyika katika Shule jijini Dar es Salaam.
Picha za pamoja za makundi mbalimbali Mara baada ya Kukabidhiana msaada uliotolewa na NIC jijini Dar es Salaam.
NIC Yaahidi kuendelea na ushirikiano katika jamii kutoa misaada ya utatuzi WA changamoto.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) limesema kuwa katika cha hivi karibuni limekuwa linafanya vizuri na kuweza kulipa kodi za serikali na kuweza kusaidia jamii katika changamoto ambazo zinakuwa kikwazo kwenye utoaji wa huduma.

NIC katika usaidiaje kwa jamii iliahidi ahadi ya kutoa kiasi cha Shilingi Milioni 26 kwa ajili ya kukarabati wa mabweni katika ya shule ya Sekondari Jitegemee,jijini Dar es Salaam ambapo imetekelezwa kwa asilimia 100.

Akizungumza katika hafla ya Kukabidhi vifaa vya Ujenzi wa ukarabati wa mabweni hayo Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa NIC ambaye ni Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika hilo Isaya Mwakifulefule amesema msaada walioutoa utawasaidia wanafunzi kupata mazingira bora ya kulala hivyo na kuendelea kufanya vizuri katika mitihani yao na kuwa faida kwa Taifa ya kuweza kupata wataalam mbalimbali wa kuweza kuendelea kufanya mabadiliko ya kiuchumi.

Mwakifulefule amesema kazi ya wanafunzi kutunza miundombinu ili kuweza kuipendezesha shule hiyo kwa kuendelea kunufaisha vizazi na vizazi kutumia miundombinu hiyo.

Aidh.Mwakifulefule amesema Shirika hilo litatuma wataalamu kwaajili ya kutoa elimu kuhusu bima ili waweze kuelewa umuhimu Bima ya NIC pamoja na kuwa mabalozi wazuri pindi wakiwa katika jamii ikiwa ni kuwa sehemu ya wanufaika na huduma za shirika hilo.

"Mkuu wa shule wiki ijayo nitatuma vijana watakuja hapa kuwapeni shule ya bima ili kuelewa namna ya kutumia huduma za bima zenye bei rahisi lakini manufaa yake ni makubwa zaidi tena vijana hao walisoma hapahapa Jitegemee". Amesema Mkurugenzi wa Masoko Mwakifulefule.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Jitegemee Kanali Robert Kessy ameushukuru uongozi wa NIC kwa kuweza kutekeleza ahadi waliyoiahidi kutoa fedha hizo zilizowezesha kununua vifaa kwa ajili ya kukarabati mabweni katika shule hiyo.

"Niwapongeze NIC kwa kuja kutukabidhi rasmi ile thamani ambayo waliahidi ya Milioni 26 tumeona mfano wa vitu ambavyo vitatumika kwenye huo ukarabati". Amesema Kanali Kessy.

Aidha amesema uamuzi huo wa kuwasaidia ulitokana na ombi lao walilowasilisha kwenye mahafali ya kidato cha sita mwaka huu ambapo waliwasilisha kutokana na hitajio baada ya kufanyika kwa ukaguzi.

Nao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wameushukuru uongozi wa NIC na kuahidi kuendelea kulinda na kuthamini mchango ambao umetolewa na shirika hilo na kuwafanya kuishi katika mazingira mazuri ya masomo.

No comments :

Post a Comment