Thursday, August 19, 2021

WAFANYABIASHARA WAKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO NCHI ZA EAC

Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki ,Peter Mathuki akizungumza katika mkutano na wafanyabiashara wa jumuiya hiyo mkoani hapa (Happy Lazaro).
*****************************
Happy Lazaro, Arusha
Arusha.Katibu Mkuu wa jumuiya ya Afrika mashariki Peter Mathuki amewataka wafanyabiashara wa Afrika mashariki kufanya Kazi kwa pamoja ili kupunguza gharama na kuweka mahusiano mazuri kwa nchi za Afrika mashariki.
Mathuki ameyasema hayo  wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika kikao Kazi kilichowakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania.
“Mimi kama katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika mashariki ninaona kikao hiki ni cha muhimu sana kwa kuwashirikisha wafanyabiashara na wadau wa sekta binafsi, ili kuona namna ya kuondoa vikwazo kwa wafanyabiashara hao ndani ya jumuiya hii” amesema Mathuki.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji baraza la biashara jumuiya ya Afrika Mashariki (EABC)John Bosco Kalisa amesema kikao hiko ni muhimu sana kwa kuwakutanisha wafanyabiashara na sekta binafsi kujadili kwa pamoja na kutoka na mitazamo ya pamoja ili kujenga baraza la biashara kwa pamoja. 
kalisa amepongeza ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa namna wanavyoshirikiana na baraza hilo la biashara huku ikiwa lengo ni kuona biashara inafanyika bila vikwazo vitakavyokwamisha wafanyabiashara kufanya kazi ndani ya jumuiya
Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amesema kuwa ,biashara kati ya nchi hizi za jumuiya kwa takribani miezi sita zimeongezeka ambapo wakuu wa nchi pamoja na watendaji wa jumuiya hiyo wanaendelea kupambana kutengeneza mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara hao.
Amesema kuwa, Arusha kama makao makuu ya jumuiya ina changamoto kubwa sana ya kuchangamkia fursa na kuwataka wafanyabiashara kuja na majawabu badala ya malalamiko na changamoto ili kufikia malengo.
“Sisi kama serikali ya Mkoa wa Arusha tunatengeneza dawati ambalo litaweza kuwahudumia na kusaidia changamoto na sio kuweka urasimu na ucheleweshwaji wa biashara” Amesema Mongela.

No comments :

Post a Comment