Monday, August 30, 2021

UHABA WA VYOMBO VYA HABARI VISIWANI PEMBA YAPELEKEA JAMII KUTOSIKIA CHANGAMOTO ZAO ZA KIBIASHARA

Mkurugenzi wa Taasisi ya The warrior Women Sabra Machano akizungumza na wajasiriamali wadogo wadogo na wakubwa katika visiwa vya Pemba katika Kongamano la pili lililopewa jina la "Tunachonga barabara la Taasisi hiyo na kubaini changamoto na shuhuda za wajasiriamali hao katika biashara zao

Wajasiriamali wanawake kutoka visiwa vya Pemba waliojitokeza katika Kongamano la pili lililopewa jina la Tunachonga barabara la Taasisi ya "The warrior Women Foundation"
Muimbaji wa qaswida Ukhty Rauhiya akitoa burudani ya utenzi wa qaswida katika Kongamano visiwa vya Pemba huku akipatiwa fedha kama pongezi kutoka kwa Mjasiriamali visiwani humo.
Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
WAJASIRIAMALI Kisiwa cha Pemba wameeleza sababu zinazopelekea kutoboresheka kwa biashara zao na kutofikika kwa Masoko ya sehemu mbalimbali hasa kisiwa cha unguja kutokana na uhaba wa vyombo vya habari katika kisiwa hicho.

Akizungumza katika kongamano la "Tunachonga Barabara" Mchoraji wa urembo (Hina) Fatma Khamis , ambapo kongamano hilo limeandaliwa na Taasisi isiyo ya kiserikali yenye kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakubwa "The warrior Women Foundation"amesema katika biashara yoyote ile lazima kuwepo na muongozo ambao utaupa mwanga biashara hiyo ili iweze kutambulika sehemu mbalimbali katika jamii lakini changamoto iliyopo kisiwa cha Pemba ni vyombo vya habari .

"Pemba Kuna Vitu vyote Pemba kama tulivozoea kutoa vitu sehemu mbalimbali kama Dar es salaam hivyo kungekuwepo kwa vyombo vya habari vikasimama kidete kwa ajili ya kujulisha watu kuwa hata Pemba vitu vipo tuunge Mkono wajasiriamali wa kwetu ingesaidia mno."

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wajasiriamali kisiwa cha Pemba, Mzee Nyuki amempongeza Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Sabra Machano kwa kuona ipo haja ya kisiwa hicho kufikiwa na kupewa elimu kwa jinsi gani wanatanua Masoko yao na kukabili changamoto ndogo na kubwa katika biashara zao.

"Kwa mara ya kwanza kufanyika kisiwa cha Pemba japo lilizinduliwa unguja lakini tumepata fursa ya kusikilizwa kero zetu,changamoto zetu kwa namna gani hatufiki tunapopataka hivyo kupitia Kongamano hili litasaidia zaidi wajasiriamali kujitambua, kufanya kazi kwa bidii, Kuboresha biashara zao kwani ipo tayari Taasisi ambayo imehaidi itashirikiana nasi bega kwa bega kuhakikisha tunapata Masoko ya kutambulisha bidhaa zetu na kuhakikisha biashara zetu zinaleta faida" Amesema.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Taasisi hiyo amewashukuru wote waliojitokeza katika Kongamano Hilo na kutoa shuhuda,changamoto pamoja na Mafanikio yao katika biashara.

"Kazi yetu kama taasisi ilikua ni kusikiliza changamoto zao pamoja na kuzifanyia utafiti kwa namna gani tunaweza kuzitatua ili kubadilisha dhamira iliyojengeka kuwa tunaweza kuagiza bidhaa kutoka sehemu tofauti wakati hapa pemba inapatikana vizuri lakini tukiweza kutatua changamoto ndogo ndogo tunaweza badilisha kabisa dhamira hiyo." Amesema.

No comments :

Post a Comment