Tuesday, August 24, 2021

RC MAKALLA: COCO BEACH KUBORESHWA, KUWA SEHEMU NZURI YA MAPUMZIKO, BURUDANI NA UTALII.

-






 
 Maboresho kufanyika muda wowote kuanzia leo.


-Asema hakuna Mfanyabiashara atakaeondolewa.

- Ajipambanua dhamira yake ya kuzifanya fukwe zote Dar kuwa sehemu ya utalii.



- Wafanyabiashara wamshukuru kwa kuwatafutia Wadau wa kujenga mabanda ya kisasa bure.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amefanikiwa kupata Wadau waliokubali kuwajengea Wafanyabiashara wa ufukwe wa Coco Vibanda vya kisasa na kuboresha mandhari ya ufukwe huo ili uwe kwenye mwonekano wa Kisasa.

RC Makalla ametembelea ufukwe huo leo akiambatana na Viongozi na Wadau waliokubali kuwa sehemu ya maboresho ya fukwe wakiwemo Bank za NMB, CRDB, Kampuni za utengenezaji wa Vinywaji zikiwemo TBL, Coca-Cola, Pepsi, Asas, Azam group na Wadau wengine.

Akizungumza na Wafanyabiashara hao RC Makalla amesema wa dhamira yake na Serikali ni kuona Coco inakuwa ya kisasa na shughuli za kiutalii zinafanyika ambapo tayari amezungumza na Mfanyabiashara mkubwa Nchini Said Salim Bakhresa kwaajili ya kuleta boti za utalii kwenye fukwe hiyo.

Aidha RC Makalla ameelekeza Manispaa ya Kinondoni kuanza Mara moja Ujenzi wa Ofisi, Stoo na vyoo vya kisasa kwenye ufukwe huo.

Hata hivyo RC Makalla ametoa maelekezo kwa Manispaa ya Kinondoni kupeleka umeme eneo lote la Coco huku akimuelekeza RPC Kinondoni Kuimarisha ulinzi kwenye ufukwe huo.

Mpango wa RC Makalla kuboresha Fukwe za Dar es salaam unaenda sambamba na maboresho ya maeneo ya Wazi, Bustani za kupumzika, Usafi na upandaji wa miti, maua na kingo pembezoni mwa Barabara.

No comments :

Post a Comment