Sunday, August 22, 2021

RAIS SAMIA APOKEA KOMBE LA CECAFA U23 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipokea Kombe la Ubingwa wa Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA U23 kutoka kwa Nahodha msaidizi wa Timu ya Taifa ya Vijana U23 Reliant Lusajo leo tarehe 22 Agosti, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali wa michezo, Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana U23, Wanariadha walioshiriki michezo ya Olimpiki (Japan) mara baada ya kupokea Kombe la Ubingwa wa Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA U23 leo tarehe 22 Agosti, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya Pamoja na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana ya U23 mara baada ya kukabidhiwa kombe la Ubingwa wa CECAFA U23 Challenge Cup leo tarehe 22 Agosti, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa pamoja na  Rais wa TFF Wallace Karia.

Baadhi ya Wachezaji wa timu ya Taifa ya Vijana U23 wakiwa katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya U23 wakiwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Agosti, 2021. (PICHA NA IKULU).



 

No comments :

Post a Comment