MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa utetezi katika kesi ya usafirishaji haramu wa binadamu inayomkabili raia wa Misri Mohamed Shalaby kuhakikisha wanakamilisha maombi waliyotoa mahakamani hapo ili kesi hiyo iweze kuendelea katika hatua nyingine.
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Issaya ameto agizo hilo leo Agosti 24,2021 wakati shauli hilo lilipoitwa kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali kufuatia upelelezi kukamilika.
Mapema kabla ya kutolewa kwa agizo hilo, upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa serikali kutoka idara ya uhamiaji, Godfrey Ngwijo alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo leo ymahakamani hapo kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali lakini siku moja kabla upande wa utetezi ulipeleka maombi ya mshtakiwa kubadili msimamo wa kukana shtaka lake.
"Mheshimiwa shauri hili limekuja kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali, lakini jana upande wa utetezi ulileta maombi ya mshtakiwa kubadili nia ya kukana mashtaka na waliomba muda waweze kujadiliana hivyo tungependa kujua wamefikia wapi," alidai Ngwijo.
Akijibu hoja hiyo Wakili wa utetezi Magusu Mugoka amedai bado wako katika majadiliano na ndugu wa mshtakiwa na bado hawajafikia muafaka hivyo waliomba tarehe nyingine.
Upande wa mashtaka ulikubaliana na ombi lao lakini waliiomba mahakama kuwa kesi hiyo itakaporejea wawe wameshakubaliana na kutekeleza ombi lao kinyume na hapo watasoma maelezo ya awali kwa mshtakiwa na kuanza kusikiliza shahidi wa kwanza siku hiyo hiyo.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Shalaby anakabiliwa na shtaka la usafirishaji haramu wa binadamu kosa analodaiwa kulitenda Agosti 4, 2021 katika eneo la makazi la Avone, Ilala, Dar es Salaam. Inadaiwa akiwa ni raia wa Misri na Mauritania alikutwa akisafirisha jumla ya watu 95. kati yao 90 ni raia Tanzania na watano ni raia wa burundi.
No comments :
Post a Comment