Thursday, August 19, 2021

MBUNIFU WA UMEME HAVANGA AOMBA KUSHIKWA MKONO NA TANESCO

  

*********************************

NJOMBE

Serikali imetakiwa kuwashika mkono wabunifu kwa kuendeleza vipaji na ujuzi wanaotumia kuvumbua vitu mbalimbali nchini badala ya kuwatelekeza ,kwakuwa kufanya hivyo kutasaidia kutengeneza ajira kwa kundi kubwa la vijana ambalo limekumbwa na tatizo hilo.

Katika kijiji cha Havanga kilichopo wilayani Njombe  kuna mbunifu wa umeme

anaefahamika kwa jina Frank Kihombo ambaye amebuni mradi wa umeme kwa kutumia njia asilia na vifaa duni na kisha kusambaza huduma hiyo kwa kaya zaidi ya 30 kijiji kwake ambapo anasema licha ya jitihada zake lakini mamlaka zimemtelekeza.

Amesema amekuwa akifanya shughuli hiyo kwa muda mrefu sasa lakini hajawahi kupewa usaidizi wa namna yeyote na watalaamu wa tanesco jambo ambalo linamkatisha tamaa ya kuendelea na ubunifu zaidi.

Mara baada ya kusikia jitihada za mbunifu huyo Prof Win Van Havarbeke kutoka chuo kikuu cha Antwerp Ubelgiji amelazimika kufika kijiji kwa mbunifu na kisha kueleza alichokiona na kujifunza.

Prof Haverbeke anasema amepita na kujionea ubunifu wa kustaajabisha katika mradi wa umeme wa bwana Kihombo na kwamba anahitaji kushikwa mkono ili aweze kufanya vizuri zaidi na kusaidia wananchi.
Katika Msafara huo pia umemhusisha Dr Nicholous Tutuba kutoka idara ya Ujasiriamali na masoko chuo kikuu cha Mzumbe ambaye pia ametoa kauli baada ya kujionea ubunifu wa mkazi huyo ulivyonufaisha wakazi ambapo amesema wataendelea kumpa ujuzi wa kitalaamu 
Zaidi ya Miaka Mitatu Kijana Frank kihombo anajishughulisha na Uwekezaji huu ambao anasema Mpaka Hivi Sasa amewekeza Zaidi ya Milioni 20 Katika Mradi Huo na kuzalisha Umeme wa Kilowati 3 .

No comments :

Post a Comment