Kaimu Mkurugenzi wa Sera,Utafiti na mipango wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana (CMSA), Alfred Mkumbo (wa pili kushoto) akikabidhi kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA hati fungani inayokidhi matakwa ya sheria za Kiislam yaani Sharia Complicant Capital Market Product (Sukuk Wakala) ya Kampuni ya Imaan Finance kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela,.Kushoto ni Afisa mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Imaan Financge Ltd,Faiz Arab pamoja na Mwenyekiti wa Bodi wa Wakurugenzi ya Kampuni ya Imaan Finance Ltd Aunali Fidahussein Rajabali (kulia) wakishuhudia tukio hilo.Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Sera,Utafiti na mipango wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana (CMSA), Alfred Mkumbo akisoma hotuba kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA,mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani) waliofika katika hafla ya MAMLAKA ya Masoko ya mitaji na dhamana (CMSA) ikitoa hati fungani inayokidhi matakwa ya sheria za Kiislam yaani Sharia Complicant Capital Market Product (Sukuk Wakala) ya Kampuni ya Imaan Finance ambapo hati za uwekezaji katika hati fungani zimetolewa rasmi.
Kaimu Mkurugenzi wa Sera,Utafiti na mipango wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana (CMSA), Alfred Mkumbo akisoma hotuba kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA,mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani) waliofika katika hafla ya MAMLAKA ya Masoko ya mitaji na dhamana (CMSA) ikitoa hati fungani inayokidhi matakwa ya sheria za Kiislam yaani Sharia Complicant Capital Market Product (Sukuk Wakala) ya Kampuni ya Imaan Finance ambapo hati za uwekezaji katika hati fungani zimetolewa rasmi.
Kaimu Mkurugenzi wa Sera,Utafiti na mipango wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana (CMSA), Alfred Mkumbo (wa pili kushoto) akikabidhi kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA hati fungani inayokidhi matakwa ya sheria za Kiislam yaani Sharia Complicant Capital Market Product (Sukuk Wakala) ya Kampuni ya Imaan Finance kwa viongozi Waandamizi wa Benki ya KCB,kulia ni Kaimu MKurugenzi Mtendaji wa KCB Bank Bi.Antonia Kilama pamoja na Mkuu wa Kitengo cha huduma za Kiislam Amour Muro (pili kulia).Kushoto ni Afisa mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Imaan Financge Ltd,Faiz Arab pamoja na Mwenyekiti wa Bodi wa Wakurugenzi ya Kampuni ya Imaan Finance Ltd Aunali Fidahussein Rajabali.Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wageni waalikwa mbalimbali waliofikwa kwenye hafla hiyo fupi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam
MAMLAKA ya Masoko ya mitaji na dhamana (CMSA) imetoa hati fungani inayokidhi matakwa ya sheria za Kiislam yaani Sharia Complicant Capital Market Product (Sukuk Wakala) ya Kampuni ya Imaan Finance ambapo hati za uwekezaji katika hati fungani zimetolewa rasmi.
Akisoma hotuba hiyo leo katika hafla hiyo kwa Niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, Kaimu Mkurugenzi wa Sera,Utafiti na mipango wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana (CMSA), Alfred Mkumbo amewashukuru wageni waalikwa na wadau wote wa sekta ya fedha kwa kuweza kutenga muda kutoka kwenye ratiba zao na kuweza kuhudhuria hafla hiyo muhimu.
Amesema utoaji wa Hatifungani ya Sukuk Wakala ya Kampuni ya Imaan Finance Limited ni matokeo chanya ya ushirikiano wa wadau katika sekta ya masoko ya mitaji wenye lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, za kuhakikisha kwamba Sekta ya Fedha inawezesha upatikanaji wa rasilimali fedha kwa Kampuni za wajasiriamali wadogo na wa kati.
Amesema hatua hiyo ni muhimu, kwani ina matokeo chanya katika ukuaji wa sekta binafsi, umma na uchumi wa nchi kwa ujumla.
" Utoaji wa Hatifungani hii ni matokeo ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) wenye lengo la kuziwezesha Kampuni mbalimbali kutumia fursa zilizopo katika masoko ya mitaji, ikiwa ni pamoja na kupata mitaji ya muda mrefu ya kugharamia miradi ya Maendeleo.
Hatua hii ni muhimu, kwani inatarajia kuongeza idadi ya wawekezaji katika masoko ya mitaji, na hivyo kuchangia utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha (National Financial Sector Development Master Plan 2019/20 – 2029/30; Mpango wa tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22–2025/26 (The Third Five Year National Development Plan (FYDP III) wenye dhima ya “Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya Watu”; na Mpango Jumuishi wa Huduma za Kifedha hapa nchini (National Financial Inclusion Framework)," Amesema.
Ameipongeza Bodi na Uongozi wa Kampuni ya Imaan Finance kwa kufanikisha uuzwaji wa Hatifungani ya Sukuk Wakala na hatimaye Hati za Uwekezaji katika Hatifungani hii zinatolewa rasmi.
Amesema kuwa CMSA iliidhinisha maombi ya Kampuni ya Imaan Finance Limited kuuza hatifungani yenye thamani ya Shilingi bilioni 2.0 kwa Mpango wa Uwekezaji binafsi yaani Private Placement kwa mujibu wa Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Sura ya 79; na Miongozo ya Masoko ya Mitaji na Dhamana ya Utoaji wa Hatifungani ya mwaka 2019, yaani “Capital Markets and Securities (Guidelines for the issuance of Corporate Bonds, Municipal Bonds and Commercial Papers), 2019”.
" Hatifungani hii imekuwa ya kwanza katika historia ya sekta ya fedha hapa nchini ambayo inayokidhi matakwa ya Sharia yaani Sharia Compliant Product.
Fedha zilizopatikana kupitia mauzo ya hatifungani hii zitatumika kutekeleza Mpango Mkakati wa kutoa mikopo kwa Kampuni zinazoendesha biashara zinazokidhi matakwa ya Sheria za Kiislam, itakayowezesha wawekezaji kugawana faida inayopatikana kwenye biashara (Profit Sharing)," Amesema.
Amesema dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, ni kuona kuwa Sekta ya Fedha inawezesha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kutoa mikopo kwa gharama
No comments :
Post a Comment