Mkurugenzi wa upande wa Africa kutoka BRAC International Bi. Ruth Okowa akisikiliza jambo kutoka kwa mmoja wa mabinti wanaonufaika na mradi wa ELA unaotekelezwa na BRAC Maendeleo Tanzania. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa BRAC Maendeleo Tanzania, Bi Susan Bipa
Mkurugenzi wa upande wa Africa wa BRAC International Bi. Ruth Okowa akikabidhi vifaa vya ujasiriamali kwa mmoja wa wasichana 86 ambao walipewa vifaa hivyo katika hafla iliyofanyika katika Chuo cha Ufundi Temeke.
Katika kumkomboa mtoto wa kike ili aweze kufikia malengo yake Shirika linapojishughulisha
na masuala mbalimbali ikiwemo kutoa mikopo kwa wanawake, kutoa elimu ya miradi BRAC Maendeleo Tanzania limetoa vyeti kwa wanafunzi 86 ambao wamehitimu Mafunzo ya kozi fupi mbalimbali za ufundi stadi.
Mafunzo
hayo yanayotolewa bure walengwa zaidi ni watoto wa kike ambao wamepata
fursa kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Mapishi, urembo, Upambaji na
ushonaji.
Akizungumza katika mahafali ya kuwatunukia vyeti
wanafunzi hao, Mkurungezi wa BRAC International Afrika, Lucy Okowa
amewataka wahitimu hao kutumia vyema Mafunzo waliyoyapata ili waweze
kutimiza ndoto zao.
Okowa amesema wanafunzi hao wamenuafaika na
Mafunzo hayo chini ya mradi wa Ela ambao umelenga kumyanyua mtoto wa
kike na kumuwezesha kumudu maisha yake kiuchumi na kijamii na
kufanikiwa kumaliza mafunzo na kupata msaada wa vifaa mbalimbali
Amesema
wanawake duniani kote wamekuwa wakisifika kwa kuwa watu wenye
ustahimilivu na kujitolea kwa nguvu zao zote katika kuhakikisha familia
zao zinasonga mbele.
"BRAC ina amini kuwa ili kuleta mabadiliko
chanya katika jamii na kuinua familia kwa ujumla ni muhimu kumwezesha
mwanamke kwa sababu daima mwanamke hashindwi na jambo"amesema
Aliwasihi
wahitimu hao wanapoanza safari ya ujasiriamali wawe makini ikiwa ni
pamoja na kuzingatia Mafunzo mbalimbali waliyoyapata katika kipindi
chote cha mafunzo.
"Ujasiriamali sio lelemama nawaomba muwe
wavumilivu chagamoto nyingi mtapitia lakini msikate tamaa kila
unapofeli nyanyuka, jifunze kutokana na makosa na uendelee kukaza mwendo
kwa sababu wanawake sio jadi yetu Kushindwa"alisisitiza Okowa
Elina
Patrick ni mmoja wa wanafunzi walionufaika na Mafunzo hayo katika eneo
la Upambaji amesema Mafunzo aliyoyapata yatamsaidia kujikwamua na
kujiajiri mwenyewe na kumuwezesha kupata kipato cha kumudu maisha yake.
"Matarajio yangu ni kufungua salooni yangu mwenyewe ambayo itanisaidia kutegeneza kipato changu mwenyewe "amesema
Naye
Habiba Sangasi alilishukuru Shirika la BRAC Maendeleo Tanzania kwa
kumuwezesha kupata ujuzi uliokuwa ni ndoto yake katika maisha yake.
No comments :
Post a Comment