Wednesday, July 7, 2021

WAZIRI MHAGAMA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUZALISHA VUADUDU CHA TBPL NA MRADI WA WHC WA NYUMBA ZA WATUMISHI MABWEPANDE, BUNJU B

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akieleza jambo alipokutana na Uongozi na Wafanyakazi wa Kiwanda cha Uzalishaji wa Viuadudu (Tanzania Biotech Production Limited) wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani Pwani kujionea mradi huo ambao uwekezaji wake unahusisha Mfuko wa hifadhi ya Jamii wa NSSF.

Sehemu ya Uongozi kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na Uongozi wa Kiwanda cha Uzalishaji wa Viuadudu (Tanzania Biotech Production Limited) wakifuatilia taarifa ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi katika kiwanda hicho.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa ameongozana na Uongozi kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na Uongozi wa Kiwanda cha Uzalishaji wa Viuadudu (Tanzania Biotech Production Limited) alipotembelea kiwanda hicho Julai 7, 2021 Kibaha, Mkoa wa Pwani.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisikiliza maelezo kutoka kwa Naibu Meneja Uzalishaji Bw. Gasper Philip Kimbi (wa pili kutoka kulia) kuhusu hatua za uzalishaji wa dawa za kibaiolojia mahususi kwa kuangamiza viliwiluwi wa aina yoyote wa mbu wanaoneza ugonjwa wa Malaria na magojwa mengine.  Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Jamal Katundu.

Mteknolojia wa Dawa Bw. John Tusiwe (kulia) akieleza jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa katika Maabara maalum ya utafiti wa dawa hizo za kibailojia. Wa pili kutoka kushoto ni Diwani wa Tangini Bw. Mfalme Kabuga.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akikagua mitambo ya kuzalisha bakteria katika kiwanda cha uzalishaji wa viuadudu (Tanzania Biotech Production Limited) alipotembelea kiwanda hicho. Kushoto ni Mbunge wa Kibaha MjiniM he. Silvestry Koka.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Watumishi Housing Limited (WHC) Dkt. Freddy Msemwa (wa pili kutoka kulia) alipotembelea mradi wa nyumba za taasisi hiyo zilizopo Mabwepande, Bunju B, Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo na viongozi kutoka Watumishi Housing Limited (WHC), Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) alipotembelea mradi huo ambao uwekezaji wake unahusisha Mfuko wa hifadhi ya Jamii wa NSSF. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Jamal Katundu.

PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(SERA, URATIBU, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

 

No comments :

Post a Comment