Friday, July 30, 2021

SERIKALI YAJIELEKEZA KUONDOA KABISA TATIZO LA USIKIVU WA RADIO IFIKAPO 2025.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha kurushia matangazo cha TBC katika kijiji cha Sesenga, wilayani Morogoro, Mkoani Morogoro. Kituo hicho kimefadhiliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote( UCSAF) hafla iliyofanyika leo Julai 30,2021 katika kijiji cha Sesenga, wilayani Morogoro,Mkoani Morogoro

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe, Innocent Bashungwa, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha kurushia matangazo cha TBC katika kijiji cha Sesenga, wilayani Morogoro, Mkoani Morogoro. Kituo hicho kimefadhiliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote( UCSAF) hafla iliyofanyika leo Julai 30,2021 katika kijiji cha Sesenga, wilayani Morogoro,Mkoani Morogoro

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF), Justina Mashiba,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha kurushia matangazo cha TBC katika kijiji cha Sesenga, wilayani Morogoro, Mkoani Morogoro. Kituo hicho kimefadhiliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote( UCSAF) hafla iliyofanyika leo Julai 30,2021 katika kijiji cha Sesenga, wilayani Morogoro,Mkoani Morogoro

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe Dkt. Faustine Ndugulile na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe, Innocent Bashungwa wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa kituo cha kurushia matangazo cha TBC Taifa na TBC FM kilichojengwa kwa ufadhili wa UCSAF. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC,Dkt. Ayub Rioba na wa kwanza kushoto ni Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Justina Mashiba.

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF), Justina Mashiba akisaini hati ya makabidhiano ya kituo cha kurushia matangazo cha TBC Kisaki kilichojengwa kwa ufadhili wa Mfuko huo.

………………………………………………

Na: Celina Mwakabwale, Morogoro Vijijini

*Mpaka sasa asilimia 66 ya maeneo ya kijeografia yanapata mawasiliano*

*Yafungua milango kwa wadau kutumia miundombinu ya Serikali*

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe, Dkt. Faustine Ndugulile amesema Wizara yake imejielekeza katika kumaliza kabisa tatizo la usikivu wa radio na simu katika maeneo

mbalimbali nchini ikiwemo maeneo ya pembezoni na mipakani mwa nchi ifikapo mwaka 2025.

Waziri Ndugulile ameyasema hayo katika uzinduzi wa kituo cha kurushia matangazo ya TBC Taifa na TBC FM kilichopo katika kijiji cha Sesenga, wilayani Morogoro, Mkoani Morogoro, kituo kilichojengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa lengo la kuboresha usikivu wa radio katika eneo hilo na maeneo ya jirani ikiwemo eneo la kimkakati katika bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere.

Amesema hadi sasa asilimia 66 ya maeneo ya kijeografia nchini yanapata huduma ya mawasiliano lengo likiwa ni kufikia asilimia 100 ifikapo mwaka 2025. Kwa upande mwingine amesema matumizi ya intanet kwa sasa ni asilimia 43 lengo ni kufikia asilimia 100 pia ifikapo 2025. Kuwa upande wa usikivu wa radio tayari Wizara kupitia UCSAF imetangaza zabuni ya kupeleka mawasiliano katika kata 190 zilizo maeneo ya mipakani.

Ili kuboresha mawasiliano ya simu na huduma zingine za utangazji katika eneo hilo, Waziri Ndugulile ameiagiza UCSAF kufanya mazungumzo na makampuni ya simu pamoja na watoa huduma za utangazaji kutumia mnara huo mpya kuwekeza katika eneo hilo ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma bora za mawasiliano ya simu na utangazaji.

Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe, Innocent Bashungwa ameipongeza Wizara kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote kwa kutekeleza kwa vitendo ilani ya CCM ya 2021-2025 kwa kuiwezesha TBC kupata vifaa vya kisasa vitakavyoisadia kupanua na kuboresha usikuvu wa radio za TBC nchi nzima.

Akizungumza kwa niaba ya Kamati ya Bunge ya kudumu ya Miundombinu, Mhe. Innocent Karogenis amesema Kamati inazopongeza wizara hizo mbili kwa kushirikiana katika kuzingatia mapendekezo yanayotolewa na Kamati.

Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Justina Mashiba asema kuwa, UCSAF imetoa shilingi milioni 450 kujenga kituo hicho cha kurushia matangazo na ununuzi wa vifaa vya kisasa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya Mfuko katika kuhakikisha mawasiliano, yakiwemo matangazo ya redio yanafika kwa watu wote nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba amesema kuwa ujenzi wa kituo hicho cha kurushia matangazo utakuwa na manufaa kwa wanananchi wa maeneo hayo pamoja na maeneo mengine ikiwemo mbuga ya Selous kwa kuwa wataanza kupokea matangazo ya TBC Taifa na TBC FM.

 

No comments :

Post a Comment