Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Profesa Elisante
Ole Gabriel, akizungumza na wadau mbali mbali wa sekta ya mifugo wakati
wa hafla ya kuwapatia vyeti wauzaji sita wa pembejeo waliochaguliwa
kushiriki kutoa huduma za Ugani kwa Wafugaji wa maeneo ya Pwani, Dar es
Salaam, Morogoro na Tanga.
Mratibu
wa Mradi wa AgResults Tanzania Dairly Productivity Challenge Neema
Mrema akizungumza wakati wa hafla ya kuwapatia vyeti wauza wa pembejeo
sita waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji
walioko maeneo ya Dar es Salaa, Pwani, Morogoro na Tanga.
Mkurugenzi
wa Uzalishaji na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Steve Michael
akizungumza wakati wa hafla ya kuwapatia vyeti wauza wa pembejeo jijini
Dar es Salaam.
Wadau
mbalimbali wa sekta ya mifugo nchini wakifuatilia hafla ya kuwapatia
vyeti wauzaji sita wa pembejeo waliochaguliwa kushiriki katika kutoa
huduma za ugani kwa wafugaji maeneo ya Pwani, Morogoro, Dar es Salaam na
Tanga.
Baadhi
ya wauza wa pembejeo waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za
ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na
Tanga wakikabidhiwa vyeti mara baada ya kufanya vizuri katika sekta
hiyo Jijini Dar es Salaam.
Na Karama Kenyunko Michuzi TV
SERIKALI
imesema kuwa, sekta ya mifugo nchini inachangia uchumi wa nchi kwa
zaidi ya asilimia 7.4 na kwamba mwaka huu wa fedha unaoisha, sekta hii
imekuwa kwa asilimia 5 lengo likiwa kufikia mara mbili zaidi kwenye
mchango wa uchumi na kuweza kufikia angalau asilimia 15 ifikapo mwaka
2025.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof.
Elisante Ole Gabriel ameyasema hayo leo Juni 30,2021 wakati wa hafla ya
kuwapatia vyeti wauzaji wa pembejeo sita waliochaguliwa kushiriki kutoa
huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaa, Pwani,
Morogoro na Tanga.
Akifafanua
namna sekta hiyo inavyokuwa Prof. Gabriel amesema uzalishaji wa maziwa
nchini umefikia bilioni 3.4 ikiwa maziwa yanayosindikwa ni lita milioni
75 hali unayoonyesha kuwa wawekezaji wengi huja kuchakata na kuleta
thamani kwani wateja wananunua maziwa ambayo yameongezwa thamani .
Amesema
takwimu zinaonesha katika lita bilioni 3.4 za maziwa, lita bilioni 2.38
yanatokana na Ng'ombe wa kienyeji hivyo, na hivyo ni lita bilioni 1.2
tu ndio ¹ zinatokana na ng'ombe wa maziwa". Amesema Prof. Ole Gabriel.
Aidha
amesema Tanzania ni nchi ya pili kwa wingi wa mifugo barani Afrika
ambapo inazaidi ya ng'ombe milioni 33.9 na mbuzi wameshafika zaidi ya
milioni 22 wakati kondoo wamefika takribani milioni 6, huku kuku wakiwa
milioni 87.7.
Kwa
upande wake Mratibu wa Mradi wa AgResults Tanzania Dairly Productivity
Challenge Neema Mrema amesema kuwa kupitia mradi huo wana matokeo mazuri
wameyaona ambapo kuna ng'ombe 558 tayari wana mimba na wengine tayari
wameshapata watoto pia kuna ng'ombe 336 ambao wameogeshwa kitaalamu na
vilevile kuna ng'ombe 62 ambao hao wamepata chanjo kuanzia mbili na
kuendelea.
"Wauza
pembejeo hawa wameweza kuwafikia wafugaji 2776 na kuuza pembejeo nne
ambazo ni vidhibiti vimelea, Chanjo, lishe uhimilishaji pia mpaka sasa
tuna ng'ombe 17,000 ambao wamepata huduma mbalimbali za lishe katika
kuongeza afya bora na pia kuweza kupata maziwa yaliyobora". Amesema
Neema
Amesema
kuwa mradi huo una malengo matatu ambapo lengo la kwanza ni kuongeza
uzalishaji na tija ya maziwa kwa wafugaji wadogowadogo, kuongeza kipato
kwa wafugaji wadogowadogo wa maziwa, kuleta uwiano sahihi na kuboresha
mifumo ya uendeshaji wa shughuli katika sekta ya maziwa .
"Washiriki
sita wa mradi huu kutoka sekta binafsi wamepata tuzo na motisha za dola
za kimarekani 27,000 kwa pembejeo 4116 zilizokamilika ili waweze
kuendelea kutoa huduma na kuongeza uzalishaji wa maziwa na kukidhi soko
la Tanzania." Amesema.
No comments :
Post a Comment