Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti (kulia) akifurahia
jambo na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo muda mfupi kabla ya
uzinduzi wa programu ya Raise the Bar au Tunyanyuke Pamoja uliofanyika
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti akizungumza wakati
wa zinduzi wa kampeni ya Raise the Bar au Tunyanyuke Pamoja uliofanyika
jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo inalenga kuyasaidia mabaa zaidi ya
2,000 katika mikoa ya Dar, Arusha Mwanza na Zanzibar.
Wafanyakazi
wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) wakiwa katika picha ya pamoja muda
mfupi baada ya uzinduzi wa zinduzi wa kampeni ya Raise the Bar au
Tunyanyuke Pamoja uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo
inalenga kuyasaidia mabaa zaidi ya 2,000 katika mikoa ya Dar, Arusha
Mwanza na Zanzibar.
Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetangaza mpango maalum wa
kuyasaidia mabaa kupambana na magonjwa ya kuambikiza ukiwamo ugonjwa wa Corona wenye thamani ya shilingi bilioni 2.3 kwa ajili ya kulinda afya za wateja pamoja na wahudumuMsaada
huu wa SBL unakuja wakati dunia ikikumbwa na wimbi la tatu la ugonjwa
wa Corona huku nchi mbalimbali zikipambana kuwakinga raia wake ili
kuhakikisha shughuli za kiuchumi zinaendelea kama kawaida.
Programu
hii inayojulikana kama “Raise the Bar” au “Tunyanyuke Pamoja”, itadumu
kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia Julai 2021 na mabaa yatapata
misaada ya vifaa na mafunzo baada ya kujiandikisha na kukidhi vigezo
maalumu kupitia tovuti ya www.diageobaracademy.com.
Kwa
mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa SBL Mark Ocitti, mpango huu wa SBL ni
mchango wa kampuni hiyo katika kuunga mkono jitihada za serikali
kuwahamasisha watu na biashara kuweka mazingira safi ili kujikinga na
magonjwa ya kuambukiza ikiwamo ugonjwa wa Corona.
“Katika
programu hii, tutayasaidia mabaa kuwa na mazingira safi na salama ili
kuweza kuwalinda wateja wanaopata huduma ya chakula na vinywaji dhidi ya
magonjwa mbalimbali kiwamo ugonjwa wa Corona. Lengo letu ni kuyafanya
yanyanyuke tena. Programu hii itayanufaisha mabaa zaidi ya 2,000 katika
mikoa ya Dar Es Salaam, Mwanza, Arusha pamoja na Zanzibar,” alieleza
wakati wa uzinduzi.
Programu
hii ni sehemu ya kampeni ya kidunia inayofadhiliwa na kampuni mama ya
Serengeti, Diageo unaolenga kusaidia mabaa kupambana na ugonjwa wa
UVIKO19. Miji mingine inayonufaika na mradi ni amoja na Nairobi,
Kampala, New York, London, Edinburgh, Dublin, Belfast, Mexico City, Sao
Paulo, Shanghai, Delhi, Mumbai, Bangalore, Sydney.
Kwa
mujibu wa Diageo, programu ya“Raise the Bar” au “Tunyanyuke Pamoja”
ilibuniwa baada ya utafiti uliofanywa kwa wenye mabaa wakitafuta namna
ya kuyasaidia kurudi kwenye biashara wakati wa kipindi cha Corona.
Vipaumbele vilivyobainishwa ni pamoja na masuala ya usafi wa mazingira,
misaada ya namna ya kufanya biashara kwa kuchukua tahadhari na vifaa
vitakavyosaidia kujikinga.
“Raise
the Bar au Tunyanyuke Pamoja, itayasaidia mabaa kwa kuyapatia
wafanyakazi wake uwezo zaidi wa kujikinga na magonjwa ya kuambukza
ikiwamo Corona na pia itatoa vifaa mbali mbali kama meza, viti, vitakasa
mikono na vifaa vingine kulingana na mazingira ya baa husika. Lengo ni
kuwahakikishia wateja usalama wa afya zao pindi wanapofika kupata huduma
ya vinywaji au chakula,”alisema Ocitti.
Programu
hii ipo wazi kwa mabaa yote, makubwa na madogo yaliyosajiliwa na ambayo
yana leseni ya kuuza pombe katika mikoa ya Dar Es Salaam, Mwanza,
Arusha na Zanzibar. Ili baa iweze kufikiriwa kupata msaada chini ya
programu hii, ni lazima iwe ikifanya biashara walau mwaka mmoja kabla ya
Corona kuingia hapa nchini.
Dirisha la maombi tayari limeshafunguliwa mabaa ili muweze kupata msaada, yanatakiwa kutembelea tovuti ya Diageo Bar Academy www.diageobaracademy.com na kujisajili. Wawakilishi was SBL watakuwa wakipita katika mabaa kwa ajili ya kuwaelekeza na kuwasaidia kuzisajili baa zenu.
“Serengeti
ikiwa kama mdau wa baishara hapa nchini inapenda kuyasistiza mabaa yote
yenye sifa katika mikoa niliyoitaja kuchangamkia fursa hii,” alisema.
No comments :
Post a Comment