Monday, June 21, 2021

WANAUME WATAKIWA KUPIMA AFYA BADALA KUJITAHIMINI KWA AFYA ZA WAKE ZAO


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira na Watu wenye Ulemavu Bw. Patrobas Katambi akibeba mtoto mgongoni kuhadhimisha siku wanaume duniani iliyowataka wanaume kubeba viatu vya akina mama kuonja adha inayowakumba akina mama wakati wa malezi ya familia.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira na Watu wenye Ulemavu Bw. Patrobas Katambi akibeba mtoto mgongoni kuhadhimisha siku wanaume duniani iliyowataka wanaume kubeba viatu vya akina mama kuonja adha inayowakumba akina mama wakati wa malezi ya familia waku mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Yasinta Mboneko akionekana kufuraishwa na hatua hiyo.

Baadhi ya wanaume waliojitokeza kuhadhimisha siku wanaume duniani wakiwa katika maandamano yao katika viunga vya Manispaa ya Shinyanga.

Baadhi ya wanaume pamoja na akina mama waliojitokeza kuunga juhudi  za akina baba  kuhadhimisha siku wanaume duniani wakiwa katika maandamano yao katika viunga vya Manispaa ya Shinyanga.

………………………………………………………

Na Anthony Ishengoma –Shinyanga.

Akina baba bado hatujawa na mabadiliko, tunapima Afya zetu kupitia hakina mama wa

wanaopima na hatujitokezi kujiunga na vikundi vya  watu wanaoishi na virusi vya ukwimu matokeo yake ni kushindwa kumeza dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI kama inavyoshauriwa.

Ni maneno ya Mzee Vedasto Mtangila mkazi wa Manispaa ya Shinyanga na Mwenyekiti wa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI Manispaa ya Shinyanga aliyoyasema jana wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanaume Duniani iliyoadhimishwa katika viwanja vya Jeshi la Zima Moto Manispaa ya Shinyanga.

Mzee Mtangila anaongeza kuwa wanaume wanapopima hawawambii wake zao juu taarifa za afya yao lakini wao wanataka wanawake wakipima watoe taarifa ya afya zao ili waweze kujua taarifa zao kupitia afya za wake zao.

Mzee Mtangila anasema hali hii inapelekea wanaume kuwapiga hata kuwaua wake zao pale wanapogundua kuwa wanaweke wanatumia ARV na hivyo kuwataka wanaume waache ukatili dhidi ya wanawake kuhusu dhana zima ya suala la maambukizi ya UKIMWI.

Naye Bw. Frank Ernest kutoka Shirika la NACOPHA anasema Shirika lake kwa kushirikiana na Mkoa wa Shinyanga wameandaa Maadhimisho hayo Mkoani Shinyanga ili kupaza sauti kwa wanaume kuvaa viatu vya akina mama ili kuyaonja magumu wanayopitia akina mama katika kulea familia.

Aidha Bw. Ernest aliviambia vyombo vya habari kuwa Maadhimisho haya yanafanyika Mkoani Shinyanga kutokana na Mkoa huo kuwa na takwimu zinazonesha kuwa 56% ya wanawake Mkoani Shinyanga hawakuwai kufaidi usichana wao kwani walitoka utotoni na kuanza maisha ya ndoa.

‘’Ni kwa takwimu hizi ndio maana tuko hapa mkoani shinyanga kupaza sauti zetu ili wanaume watambue kuwa sula la malezi ya watoto ni jukumu letu sote ni sio la kuachia mama peke yake na hivypo tuvae viatu vya akina mama ili tujue magumu wanayopitia katika kulea watoto.

Bi. Sabrina Majikata Meneja Miradi Shirika la ICS anaangazia kuwa ni jukumu letu sote kumpatia mtoto haki za msingi na kuhakikisha mtoto anashiriki katika baadhi ya majukumu ya familia lakini sio kumtuma mtoto mitaani kufanya biashara labda tu kama mtoto atapenda hivyo kwa lengo la kujipatia maarifa.

Wakati huo huo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira na Watu wenye Ulemavu Bw. Patrobas Katambi ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi wa maadhimisho hayo alisema wanaume wanatumika tu katika kukalipia na kutoa adhabu na hivyo kujiweka mbali na upendo wa watoto wao.

‘’Watoto wanapenda mama zao sio kwa bahati mbaya ni kwasababu wakonao muda mwingi tofauti na wanaume ambao wanatumika tu pale mama anapotaka kuwashitakia kosa na watoto kuwachukulia wanaume kama watu wanaotisha’’. Aliongeza Waziri Katambi.

Maadhimisho ya Siku ya Wanaume Duniani inaanza tangu mwaka 1910 kuenzi mchango wa mazazi wa kiume Nchini Marekani aliyelea watoto sita peke yake baada ya mzazi mwenzake kupoteza maisha na kuchukua jukumu la kulea watoto wake kwa kuwapatia haki zote za Msingi.

 

No comments :

Post a Comment