Tuesday, June 8, 2021

WAKUU WA JESHI LA POLISI(W) WAPEWA ELIMU YA MIUNDOMBINU YA GESI ASILIA

***********************************

Wakuu wa Jeshi la Polisi wa Wilaya (Dar es Salaam,Mkuranga, Rufiji na Kilwa) inakopita miundombinu ya gesi asilia leo Tarehe 08/06/2021 wamepata wasaa wakutembelea BVS1( Block Valve Station) na PRS iliyoko Msijute Mtwara kwa ajili ya kujifunza na kupata elimu ya miundombinu ya gesi asilia.

Vilevile Wakuu hao wa Polisi waliweza kujionea jinsi miundombinu ya gesi asilia majumbani

ilivyounganisha kwenye mojawapo ya nyumba 125 za Bandari Mtwara zinazotumia gesi asilia kama nishati ya kupikia.

Aidha ziara hiyo ya kujifunza kwa Wakuu hao inaendelea kwa siku tatu mkoani Mtwara kwenye visima vya gesi asilia Mnazibay Msimbati na kituo cha kusafirisha gesi Madimba.

 

No comments :

Post a Comment