Meneja wa Maendeleo ya Biashara ya Benki ya NBC Tanga Aljiran Mbwani akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maonyesho
ya biashara ya Tanga
Meneja wa Maendeleo ya Biashara ya Benki ya NBC Tanga Aljiran Mbwani wakati wa maonyesho
ya biashara ya Tanga akipokea cheti kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Hassani Mnyima
Meneja wa Maendeleo ya Biashara ya Benki ya NBC Tanga Aljiran Mbwani wakati wa maonyesho
ya biashara ya Tanga kulia akitoa elimu kwa mkazi wa Jiji la Tanga aliyetembelea banda lao
…………………………………………………………………..
WAKULIMA
wadogo wadogo waliopo kwenye vikundi vya Ushirika (Amcos) wanatarajiwa
kunufaika na mikopo ya Kilimo inayotolewa na Benki ya ya Taifa ya Biashara (NBC)
ili kuweza kuwa na akauti za benki na kuweza kujikwamua kiuchumi.
Hayo
yalisemwa na Meneja wa Maendeleo ya Biashara ya Benki ya NBC Tanga Aljiran Mbwani wakati wa maonyesho
ya biashara ya Tanga ambapo alisema wameingia mkataba na benki ya wakulima
(TADB) na wametenga kiasi cha Bilioni
200.
Alisema fedha
hizo ni kwa ajili ya wakulima wadogo wadogo na wanaowaangalia wale waliopo
kwenye vukundi vya vyama vya ushirika (AMCOS)wanawasaidia kwa sababu taarifa
zao zinakuwa
Meneja huyo
alisema walichopeleka kwenye maonyesho
hayo ni akauti kwa ajili ya wakulima kama dhima ya mwaka huu ya kilimo ndio msingi wa viwanda inavyosema
kuwawezesha wakulima waweze kuwa na akauti za benki walau waweze kutimiza vigezo moja wapo wakati wakihitaji kupata
mikopo.
Alisema kwa
hiyo mkulima atakapokuwa na akauti hizo ambazo zinaghamara nafuu atakuwa na
uwezo wa kufanya miamala ya kibenki lakipi pia kuweza kupata fursa ya kupata mikopo
midogo na mikubwa .
“Kwanza tulianza
na wakulima wakubwa tulikuwa wanawapatia matrekta lakini pia tumeingia mkataba
na benki ya TADB na tumetenga kiasi cha
Bilioni 200 kwa ajili ya wakulima wadogo wadogo kupitia Amcos hivyo nitoe wito kwa
wakulima wakubali kufungua akauti benki na manufaa yake ni makubwa na yajayo
yanafurahisha kupitia shughuli zapo za kilimo watanufaika na huduma nzuri za
benki na mikopo mwisho wake kuweza kukuza kipato kwenye biashara zao”Alisema.
No comments :
Post a Comment