KATIBU mkuu wa wizara ya maji,Antony Sanga
akizungumza katika mkutano huo wa jukwaa la wadau wa bonde la Pangani
Leo jijini Arusha (Happy Lazaro).
Mkurugenzi wa bonde la Pangani ,Segule
Segule akizungumza na wadau mbalimbali katika mkutano huo unaofanyika
jijini Arusha leo.(Happy Lazaro)
**********************************
Happy Lazaro, Arusha.
Arusha.Wadau wa
jukwaa la Bonde la Pangani wametakiwa kuhakikisha wanatoa ushirikiano
katika kutoa elimu ya kutosha kuwaelimisha wananchi juu ya utunzaji wa
vyanzo vya maji katika maeneo yao.
Hayo yamesemwa
leo na Katibu wa wizara ya Maji ,Antony Kasanga wakati akifungua
mkutano wa wadau wa jukwaa la bonde la Pangani linalofanyika jijini
Arusha na kuwashirikisha wadau mbalimbali.
Aidha mkutano huo
una lengo la kujadiliana matatizo na fursa zilizopo katika bonde la
Pangani huku akisema kazi ya bodi hiyo ni kubwa ,hivyo bila ushirikiano
wa wadau ni ngumu kufanyika kwa utekelezaji wenye tija.
“kazi ya Bodi ni
kupima, kutunza na kugawa maji lakini kila mmoja wetu ana wajibu wa
kutoa ushirikiano katika hili hasa tukikumbuka kuwa vyanzo vya maji
haviongezeki ila vizazi vinaongezeka hivyo mahitaji ya matumizi ya maji
ni makubwa ,tunachopaswa kufanya ni kuvilinda kwa kuwaelimisha wananchi
juu ya uvamizi na uchafuzi wa vyanzo hivi” amesema Kasanga.
Kasanga ameongeza
kuwa,jukumu la wizara ya maji ni kuhakikisha wananchi wanapata maji
safi na salama lakini pia uendelezaji wa rasilimali maji kuwa endelevu
ili kuhakikisha uhaba wa maji unakuwa historia ambapo amesema wizara
pekee haitatosha kubeba majukumu hayo bali ni kila mmoja kuwajibika
katika hayo.
Naye Mwenyekiti
wa jukwaa hilo Taifa Mhandisi Mbogo Futakamba amesema ni hatua kubwa
kuwa na jukwaa ambalo kwa sasa limeanza mikutano yake kisheria huku
akisema mkutano huo ndio wa kwanza tangu kuundwa kisheria kwa jukwaa
hilo ambalo kupitia jukwaa hilo wanatarajia kujadili namna bora ya
utatuzi wa migogoro katika mabonde tisa huku na kuwa tayari mabonde
saba yameshaanza mpango wa utekelezaji wa hatua hizo.
Mkurugenzi wa
rasilimali za maji ,George Lugomela alitaja malengo mengine ya mkutano
huo kuwa ni kujenga uelewa wa rasilimali za maji , kujadili
upatikanaji wa fedha za kuendesha jukwaa hilo na Usimamizi wa maji,
pamoja na kuchangiza utunzaji wa vyanzo vya maji.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Bonde la Pangani ,Segule Segule amesema halmashauri 22
zipo chini yake kwa maana ya kanda ya kaskazini ambazo zinahitajika
kusimamiwa vizuri ili kuwa na rasilimali maji endelevu hivyo umuhimu wa
mkutano huo una nafasi kubwa kwa wadau wa maji.
” lengo letu ni
kutunza rasilimali ziwe endelevu katika Halmashauri zote za kanda ,
lakini pia tunalenga kushirikishana matatizo na fursa zilizopo katika
Bodi ya Maji bonde la Pangani katika Jukwaa hili” amesema Segule.
No comments :
Post a Comment