Mkurugenzi
wa Kampuni ya Kufua Umeme (IPTL), Herbinder Seth akitoka katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo mara baada ya mahakama hiyo kuruhusu
upande wa Jamhuri ufanye mazungumzo na Seth kutokana na barua
alizoziandika.
Na Karama Kenyunko Michuzi TV
UPANDE
wa Jamuhuri katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mkurugenzi wa
Kampuni ya Kufua Umeme (IPTL), Herbinder Seth, umeiomba Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu ufanye mazungumzo na Seth, ili wapate ufafanuzi wa
barua alizoandika kupitia wakili wake.
Hata hivyo, Mahakama imekubali ombi hilo na kuuruhusu upande wa Jamuhuri kufanya mazungumzo na mshtakiwa.
Mshtakiwa
Seth peke yake ameletwa mahakamani hapo leo Juni 10, badala ya Juni 17,
2021 kama mahakama ilivyokuwa imepanga ambapo alitakiwa kuletwa pamoja
na washtakiwa wenzake, James Rugemalira ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni
ya VIP na Wakili wa kujitegemea, Joseph Makandege, kufuatia maombi dhidi
yake ya upande wa mashtaka.
Mapema
wakili wa Serikali Mkuu, Martenus Marandu akisaidiana na Wakili wa
Serikali Mwandamizi, Ladslaus Komanya walidai mbele ya Hakimu Mkazi
Mkuu, Huruma Shaidi kuwa Seth aliandika barua yeye binafsi kupitia
wakili wake hivyo upande wa mashtaka umeona ni vema wakaja mbele ya
Mahakama kuomba kibali cha kukutana na Seth ili waweze kuzungumza nae
pamoja na wakili wake, kwa ajili ya kupata ufafanuzi wa barua hizo na
kile ambacho amedhamilia kwa dhati kifanyike.
Hata hivyo, upande wa utetezi haukuwa na pingamizi juu ya ombi hilo la mteja wao kufanya mazungumzo na upande wa Jamuhuri.
Aidha,
Wakili Marandu ameiomba Mahakama kuipanga kesi hiyo itajwe kesho ili
wapeleke mrejesho wa kile ambacho watakuwa wamezungumza.
Hakimu
Shaidi ameridhia ombi hilo na kusema..., "Mtaenda kuongea kama
mlivyoomba, na kesho mtaleta mrejesho, mshtakiwa utakaa mahabusu."
Amesema Hakimu Shaidi.
Awali,
Mahakama hiyo ilielezwaa kuwa, mazungumzo ya makubaliano ya kumaliza
kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Seth yanasuburi muongozo wa
Mkurugenzi mpya wa Mashtaka nchini (DPP).
Wakili
wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Saimon alidai, mazunguzo ya kumaliza
kesi dhidi ya mshtakiwa (Seth) yanaendelea yalipoishia, ambapo
wanasuburi muongozo kutoka kwa DPP mpya aliyeteuliwa hivi karibuni na
rais ili waweze kuwakilisha mahakamani hapo.
"Mazungumzo yanaendelea wanasubiri mwongozo wa DPP mpya ya umaliziaji wa mazungumzo yaliyokuwa yameanza." Alidai Wankyo
Awali
Seth na Wakili wa Kujitegemea Joseph Makandege waliwasilisha ombi kwa
DPP wakionesha nia yao ya kutaka maliza kesi kwa kukiri makosa yao
lakini, Mei 6, 2021 wakili huyo aliondoa nia yake ya kufanya makubaliano
na DPP akieleza kwamba mazungumzo hayo yamechukua muda mrefu
kukamilika.
Mbali
na Seth na Makandegs mshtakiwa mwingine ni mfanyabiashara James
Rugemalira ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP, wanadaiwa kutenda
makosa hayo katika Jiji la Dar es Salaam na nchi za Afrika Kusini, Kenya
na India.
Washtakiwa
wanakabiliwa na mashtaka 12 yakiwemo ya utakatishaji fedha, miongoni
mwa mashtaka hayo yapo ya kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu,
kughushi na kutoa nyaraka za kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya
udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani
22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.
Washtakiwa
wanadaiwa kati ya Oktoba 18 ,2011 na Machi 19, 2014 jiji Dar es Salaam
walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia
fedha kwa njia ya udanganyifu.
Mwanasheria Makandege, anakabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kuisababishia Serikali hasara ya Dola za Marekani 980,000.
No comments :
Post a Comment