Wednesday, June 16, 2021

TANZANIA NA MAREKANI KUSHIRIKIANA KUEPUKA MAGONJWA YASIOAMBUKIZA KWA KUHAMASISHA MAZOEZI




 WAZIRI wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amesema Tanzania na Marekani zitashirikiana kuhamasisha utoaji wa  Elimu ya afya kwa umma juu ya kujenga tabia ya kufanya mazoezi na lishe bora ili kuepuka magonjwa yasiyoambukiza ambayo yanakuwa kwa kasi sana Nchini.

 

Mhe.Bashungwa ameyasema hayo Juni 16,2021 Jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani hapa nchini Donald Wright kuhusu kukabiliana na tatizo hilo pamoja na mambo mengine yanayoigusa Wizara hiyo ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

 

"Nimemwambia Mhe. Balozi Donald kuwa  tayari Wizara yangu  inajadiliana na Wizara ya Afya kushirikiana kufanya kampeni endelevu nchi zima, Bara na Visiwani kuhusu ufanyaji mazoezi kwa wananchi." amesema Mhe.Bashungwa.

 

Aidha, Mhe. Bashungwa amesema nchi hizo zitaendelea ushirikiana kuendesha tasnia ya Sanaa na Michezo, ambapo Mhe Balozi wa Marekani Nchini amekubali ujumbe wa NBA kutoka Marekani kutembelea Tanzania mwaka huu kujadili maendeleo ya mchezo wa kikapu (basketball nchini)

 

Nae Balozi wa Marekani Nchini amemshukuru Mhe. Bashungwa kwa kuweza kupata muda wa majadiliano na amempongeza kwa kuzidi kuaminiwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kupewa dhamana yakuzidi kuiongoza wizara na kuahidi kuendelea kushirikiana kwa ukaribu ili kuleta maendeleo ya Wizara na Nchi kiujumla.







 

 

No comments :

Post a Comment