Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof.Abel Makubi akiwa na Naibu Mwakilishi Mkazi kutoka Korea Foundation for International Healthcare(KOFIH),Bi.Kim Jungyoon Kwenye ofisi za Wizara zilizopo mji wa Serikali Mtumba.
Katibu Mkuu Prof.Makubi akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya KOFIH kutoka Korea ya Kusini Bw.Ha,Seung Rae(kushoto) na Naibu Mwakilishi Mkazi Bi.Kim Jungyoon(katikati) wakati wa kutia saini makubaliano ya mashirikiano Kati ya Wizara ya Afya na Taasisi hiyo
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Idara
Kuu Afya Prof.Abel Makubi, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Bw. Ha
Seung Rae, Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya Serikali ya Korea Kusini
(Korea Foundation for International Healthcare-KOFIH) Kwenye ofisi za
wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Katika
mazungumzo yao pia wametia saini makubaliano mapya baina ya nchi hizo
mbili Katika maeneo mapya ya ushirikiano ikiwemo mafunzo na kuijengea
uwezo maabara ya Taifa ya Jamii.
Prof. Makubi ameishukuru Taasisi
hiyo kwa ushirikiano uliopo na kuendelea kuisaidia Serikali na ameahidi
miradi yote itaendelezwa vizuri ili kuleta manufaa kwa nchi.
Hata
hivyo Prof.Makubi ametumia muda huo kwa kuwashukuru KOFIH kwa
ushirikiano wao na Serikali Katika kipindi Cha kukabiliana na janga la
Corona mwaka jana.
KOFIH ni Taasisi iliyopo chini ya Wizara ya
Afya nchini Korea Kusini ambapo inashirikiana na Wizara ya Afya Tanzania
Katika maeneo ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya afya, Mradi wa kutoa
ushauri, mafunzo kwa wataalam pamoja na mafunzo kwa upande wa injinia wa
vifaa tiba.
No comments :
Post a Comment