Katibu Mkuu Prof.Makubi akiwa na Viongozi kutoka KOFIH mara baada ya kutia saini maeneo ya mashirikiano baina ya nchi hizo mbili
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof.Abel Makubi akiwa na Naibu Mwakilishi Mkazi kutoka Korea Foundation for International Healthcare(KOFIH),Bi.Kim Jungyoon Kwenye ofisi za Wizara zilizopo mji wa Serikali Mtumba.
Katibu Mkuu Prof.Makubi akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya KOFIH kutoka Korea ya Kusini Bw.Ha,Seung Rae(kushoto) na Naibu Mwakilishi Mkazi Bi.Kim Jungyoon(katikati) wakati wa kutia saini makubaliano ya mashirikiano Kati ya Wizara ya Afya na Taasisi hiyo
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Idara Kuu Afya Prof.Abel Makubi, leo
amekutana na kufanya mazungumzo na Bw. Ha Seung Rae, Mwakilishi Mkazi
wa Taasisi ya Serikali ya Korea Kusini (Korea Foundation for
International Healthcare-KOFIH) Kwenye ofisi za wizara zilizopo Mji wa
Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Katika mazungumzo yao pia wametia
saini makubaliano mapya baina ya nchi hizo mbili Katika maeneo mapya ya
ushirikiano ikiwemo mafunzo na kuijengea uwezo maabara ya Taifa ya
Jamii.
Prof. Makubi ameishukuru Taasisi hiyo kwa ushirikiano
uliopo na kuendelea kuisaidia Serikali na ameahidi miradi yote
itaendelezwa vizuri ili kuleta manufaa kwa nchi.
Hata hivyo
Prof.Makubi ametumia muda huo kwa kuwashukuru KOFIH kwa ushirikiano wao
na Serikali Katika kipindi Cha kukabiliana na janga la Corona mwaka
jana.
KOFIH ni Taasisi iliyopo chini ya Wizara ya Afya nchini
Korea Kusini ambapo inashirikiana na Wizara ya Afya Tanzania Katika
maeneo ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya afya, Mradi wa kutoa ushauri,
mafunzo kwa wataalam pamoja na mafunzo kwa upande wa injinia wa vifaa
tiba.
No comments :
Post a Comment