Sunday, June 20, 2021

TAARIFA MPYA KUHUSU CORONA,WIZARA YATOA TAHADHARI KUNA UWEZEKANO KUTOKEA WIMBI LA TATU LA MAAMBUKIZI NCHINI

…………………………………………………………………………..

Ndugu wanahabari;  

Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  inapenda kuwakumbusha tena na kuwatahadharisha wananchi wote Tanzania kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa COVID-19.  Tahadhari hii ya leo inatokana na hali ya mwenendo wa ugonjwa  huu duniani na

ongezeko la maambukizi katika nchi za Afrika  zikiwemo nchi jirani zinazotuzunguka ambazo zimekumbwa na  wimbi la tatu la mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 ambapo  maambukizi yameendelea kuongezeka maradufu kuliko ilivyokuwa  katika wimbi la pili. Hivyo wizara inawakumbusha wananchi wote  kutopuuza ugonjwa huu wa COVID-19. 

Ndugu wanahabari, 

Wizara imeanza kuona viashiria vya kutokea kwa wimbi la tatu la  mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 katika nchi yetu. Hii ni Kutokana  taarifa za ufuatiliaji wa mwenendo wa ugonjwa huu zinazofanywa 

Page 1 of 5 

na wizara na mwingiliano wa watu wetu na watu wa mataifa jirani  na mengine duniani katika shughuli za kijamii na kiuchumi.  Ndugu wanahabari, 

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani, inayotolewa  katika jarida la wiki ya 24 inayoanzia tarehe 7 hadi 13 Juni 2021,  katika kanda ya Afrika, idadi ya wagonjwa wa COVID-19 imekuwa  ikiongezeka kwa wiki tano mfululizo mfano katika wiki moja iliyopita  nchi za Afrika Kusini, Uganda, Zambia, Namibia, DRC, Angola na 

nyinginezo zimeendelea kuonyesha kuongezeka kwa idadi ya  wagonjwa isiyoshuka huku ikiripotiwa nchi hizo kukumbwa na anuai  ya virusi vipya ambavyo vinasababisha ugonjwa wa COVID-19  kuwa mkali zaidi na pia kuathiri hata watu wenye umri 

Ndugu wanahabari;  

Jukumu la kinga dhidi ya ugonjwa huu ni la kila mmoja wetu,  hivyo tusiwe na hofu ila tuendelee kuzingatia afua za kinga  Hivyo, Wizara inawataka Viongozi wote wa serikali ngazi zote,  sekta binafsi, Viongozi wa Kijamii na madhehebu ya dini  kuwajulisha wananchi wote kuchukua tahadhari zote muhimu, 

kuelimisha, na kutekeleza afua za kujikinga na tishio la wimbi la tatu  la mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19.  

Ndugu wanahabari;  

Kama tunavyofahamu, Kamati Maalum iliyoundwa na Mh. Samia  Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, , 

Page 2 of 5 

ilishauri hatua madhubuti ziendelee kuchukuliwa ambapo pia  ilielezea kufuatilia kwa karibu viashiria vya kutokea kwa wimbi la  tatu la ugonjwa wa COVID-19 nchini. Napenda kuwajulisha kuwa  serikali imeendelea kufanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa  na kamati na hivi karibuni mtajulishwa hatua za utekelezaji wake. 

Hivyo napenda kuwakumbusha na kuwasisitiza wananchi wote kutekeleza yafuatayo katika kujikinga na ugonjwa wa COVID-19; 1. kuendeleza tabia ya kunawa mikono mara kwa mara kwa  maji safi tiririka na sabuni maeneo yote na iwapo maji tiririka  na sabuni hakuna, basi tutumie vipukusi (sanitizer) katika  maeneo yote 

  1. Uvaaji wa barakoa safi na salama, ambayo umetengeneza  mwenyewe au umenunua kwa watengenezaji wa ndani ya  nchi yetu, waliothibitishwa na niwaombe watalam wa afya  kutoa elimu juu ya uvaaji sahihi wa barakoa. Barakoa  zivaliwe katika maeneo yote yenye msongamano wa watu. 
  2. Kuepuka misongamano isiyo ya lazima ikiwemo kwenye  vyombo vya usafiri, kwenye misiba, makanisani, kwenye  mipira na hivyo kuzingatia kukaa umbali wa mita moja au zaidi  kutoka mtu mmoja na mwingine na kuhakikisha maeneo hayo  yanakuwa na mzunguko wa hewa wa kutosha 

Page 3 of 5 

  1. Kufanya mazoezi mara kwa mara, kulingana na hali ya afya  ya mtu, na mazingira aliyonayo, kama vile kutembea kwa kasi, si chini ya dakika 30 au zaidi, hadi kutoka jasho, kuruka  kamba, kukimbia mwendo unaoona unakufaa na kufanya  zoezi popote ulipo.  
  2. Kuzingatia lishe bora inayojumuisha matunda na mboga za  majani zinazopatikana nchini kwa gharama nafuu, kulingana  na mazingira ya vyakula vya asili katika eneo analoishi mtu.  
  3. Kwa wale wenye umri mkubwa, wenye uzito uliopitiliza na  wenye magonjwa sugu kama Pumu, Shinikizo la juu la Damu,  Kisukari, Magonjwa ya Moyo na Figo kuchukua hatua  madhubuti 
  4. Kuwahi matibabu kwenye vituo cha kutolea huduma za afya,  mara waonapo dalili za ugonjwa wa UVIKO-19 kama Mafua  Makali, Maumivu ya koo, Maumivu ya kichwa, Uchovu wa  Mwili, Kupumua kwa shida, Kukosa Hamu ya Kula na  Kupoteza uwezo wa Kunusa harufu mbalimbali. 

Ndugu wanahabari;  

Wizara inapenda kuwakumbusha tena Wakuu wa Mikoa na Wilaya,  Viongozi wa wizara zote, Wakuu wa taasisi za umma na binafsi,  Viongozi wote wa dini na kijamii kuchukua hatua za kiuongozi katika  kuelimisha, kuratibu na kusimamia jamii katika kuchukua tahadhari. 

Aidha, wizara inawataka Waganga wakuu wa Mikoa na 

Page 4 of 5 

Halmashauri na Maafisa Afya wanaotoa huduma mipakani  kuendelea kuimarisha udhibiti wa magonjwa katika maeneo hayo  kwa mujibu wa miongozo husika. Pia, kuendelea kufuatilia  magonjwa na matukio hatarishi kwa afya kwenye maeneo yao, ikiwa  ni pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa Umma kuhusu namna ya  kujikinga. Vilevile inawasisitiza kuratibu kwa karibu taarifa zote za  magonjwa ya milipuko pamoja na magonjwa mengine mbalimbali  na kutoa taarifa hizo kupitia mfumo wa ufuatiliaji mwenendo wa  magonjwa nchini.  

Mwisho Wizara inawakumbusha wananchi kuendelea kutoa taarifa  zozote za kiafya na kupata ufafanuzi wa masuala ya kiafya na  magonjwa ya mlipuko kupitia namba ya simu 199 bila malipo yoyote na kuwasihi wananchi kufuatilia na kuzingatia taarifa za  mwenendo wa ugonjwa huu kutoka vyanzo rasmi vya serikali.  

 

No comments :

Post a Comment