MKUU
wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla leo amefanya kikao cha pamoja na
Maafisa Afya na Mazingira kutoka Wilaya tano za Mkoa huo kwa lengo la
kujadiliana hatua za mwisho za ukamilishaji wa Mpango Mkakati wa
kuifanya Dar es salaam kuwa Safi.
Katika kikao hicho RC Makalla alitaka kujua ni mambo gani yamekuwa kikwazo kwao hadi kusababisha Jiji kuwa Katika hali ya uchafu na nini kifanyike ili kampeni ya usafi inayopangwa kuanza hivi karibuni iweze kuwa na mafanikio makubwa.
RC
Makalla amesema lengo lake ni kuona Dar es salaam inakuwa katika hali
ya usafi kwakuwa Jiji hilo linabeba taswira ya Nchi na ndilo linalopokea
wageni wa mataifa mbalimbali hivyo ni lazima liwe kwenye hali ya
usafi.
No comments :
Post a Comment