wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF)
Ally Mwakababu kushoto akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Viwanda na
Biashara Exaud Kigahe (MB) wakati alipotembelea Banda lao lililopo
kwenye maonyesho ya Biashara ya 8 yanayoendelea kwenye viwanja vya
Mwahako Jijini Tanga
Meneja
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu
katika akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa mfuko huo kwenye
banda lao kulia ni Afisa Matekelezo wa NHIF mkoa wa Tanga Macrina
Clemence
NA OSCAR ASSENGA, TANGA.
MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF)
Ally Mwakababu amewahamasisha wakazi wa mkoa huo kuchangamkia fursa ya kujiunga
na mfuko huo ili kuweza kujihakikishia kupata huduma za matibabu wanapoungua na
hivyo kuwaondolea wasiwasi akiugua itakuwaje.
Mwakababu aliyasema hayo wakati akiwa eneo la Mwahako Jijini
Tanga kunakoendelea maonyesho ya nane ya Biashara ambapo alisema kuwa na kadi
ya bima ni kuwa na daktari hivyo inakusaidia kukuondolea wasiwasi pindi
unapougua huku ukiwa hauna fedha.
Alisema hivyo wananchi wanapaswa kutambua umuhimu wa
kujiunga na mfuko huo na kuweza kunufaika na huduma mbalimbali za kimatibabu
pindi wanapougua
Meneja huyo alisema wameshiriki kwenye maonyesho hayo ya
biashara ya TCCIA kwao wanaamini bima ya afya kwa wote serikali ya awamu ya
sita inapambana kuhakikisha watu wanajiunga na bima ya afa badala ya kusubiri
kupata matibabu kulipia.
“Kwa hiyo ndio maana tupo hapa kutoa elimu kwa wanachama na
ushauri wa afya zao kwa kupima uzito,presha,sukari na kushauri mwenendo mzuri
wa kula na kuwaeleza umuhumi wa kujiunga na bima”Alisema
Alisema pia ikiwemo Toto Afya Kadi na makundi mbalimbali ambayo
serikali imeyaweka kwenye mpango ambao ni wakulima kupitia Amcos zao,waandishi
wa habari katika eneo lao walipe laki moja,makundi ya wavuvi,warina asali na
watu binafasi wa na vifurushi mbalimbali ikiwemo najali,timiza.
Hata hivyo aliwaomba wananchi wajiunge na wafike na
kuchangmkia fursa za kujiunga na mfuko huo kwani kuwa na kadi ya bima inakuhakikishia
kupata matibabu .
No comments :
Post a Comment